Streptomyces scabies
Bakteria
Hakuna dalili zinazoonekana kwenye sehemu za juu za mmea kama vile majani, mashina au vikonyo. Kawaida, ishara za kwanza za ugonjwa huo huonekana kwenye uso wa viazi vichanga na hupanuka v inapokua na kusababisha dalili zifuatazo: kutu ya juu juu ambayo inaenea sehemu kubwa ya ngozi, ngozi nyekundu-kahawia yenye magaga yaliyoinuka, yenye rangi nyeusi, mashimo yenye kina zaidi au kidogo, na mfululizo wa nyufa zinazofanana na wavu. Zaidi ya aina moja ya vidonda vinaweza kuwa kwenye kiazi kimoja. Mazao mengine ya mizizi na mzizi mkuu yanaweza kuathiriwa, kama viazi-sukari, karoti, parsnip na radish. Katika hali zote husababisha kupungua kwa ubora wa mizizi na hasara ya mavuno.
Matibabu ya mimea ya viazi kwa mboji, chai ya mboji au mchanganyiko wa vyote kwa kiasi kikubwa hupunguza ukali wa ugonjwa wa kawaida wa kigaga cha viazi. Mbolea ya kibaiolojia yenye aina za bakteria zinazoshindana inaweza kuongeza mavuno na ubora wa kiazi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali ya kigaga cha viazi ni magumu, kwa sababu mara nyingi husababisha majeraha ya mimea. Matibabu ya mbegu kwa fluazinam, chlorothalonil na mancozeb yalionyesha asilimia ndogo ya maambukizi.
Dalili husababishwa na bakteria aitwae Streptomyces scabies, ambae huishi kwenye tishu za mizizi iliyoambukizwa kwenye udongo. Anasambazwa kupitia maji, kwenye mimea iliyoambukizwa, na kwenye udongo unaopeperushwa na upepo. Anaingia kwenye tishu za mmea na tunguu hasa kwa njia ya majeraha na matundu ya asili. Hali ya hewa kavu na ya joto wakati wa ukuaji wa mizizi huongeza hatari ya kuambukizwa. Kwa kuwa bakteria wanahitaji kiasi kikubwa cha oksijeni, uwezekano wa kuambukizwa ni mkubwa katika udongo ulio legea na wenye hewa ya kutosha. Bakteria huenea zaidi kwenye udongo mkavu na wa alkali. Aina za viazi pia hutofautiana katika kukabiliwa na bakteria wa S. scabies na baadhi ya mimea sugu imeonekana kuwa na lentiseli chache, ngumu na ngozi nene.