Pseudomonas syringae
Bakteria
Madoa madogo ya mviringo huonekana mwanzoni kwenye majani. Madoa haya baadaye yanakua na kuwa mabaka makubwa, yenye umbo la pembe hadi yasiyo na umbo maalumu, na yenye unyevu. Katika hali ya hewa ya majimaji, matone ya ute unaotolewa na bakteria hutoka kwenye madoa upande wa chini wa majani. Matone haya hupoteza unyevunyevu na kutengeneza gamba jeupe wakati wa hali ya hewa ya ukavu. Baadaye, maeneo yaliyoathirika tishu zake ufa, hubadilika rangi na kuwa ya kijivu na kunyauka, mara nyingi yakichanika kutoka kwenye tishu za jani zenye afya na kuanguka. Majeraha haya mara nyingi huwa na kingo za manjano. Mashimo makubwa na yasiyo na umbo maalumu yanasababisha majani kuwa na muonekano kuraruka. Kwa baadhi ya aina ya mimea inayostahimili ugonjwa, majeraha huwa madogo na hayana kingo za manjano. Matunda yaliyoathirika yanaonyesha madoa madogo ya mviringo ambayo mara nyingi hutokea juu juu. Tishu zilizoathirika zinapokufa, hubadilika rangi na kuwa nyeupe na kisha kupasuka, na hivyo kuruhusu vijidudu nyemelezi vya kuvu/ukungu na bakteria kukalia maeneo hayo na kusababisha kuoza kwa tunda lote. Maambukizi ya matunda machanga yanaweza kusababisha kuanguka kwa matunda kwa kiwango kikubwa.
Mbegu zilizoathirika zinaweza kutibiwa kwa kutumia mchanganyiko wa vitunguu saumu na maji ya moto (50°C) kwa dakika 30. Katika nyumba kitalu, kutokea kwa Doa Pembe la Matango kunaweza kupunguzwa kwa kudhibiti unyevunyevu wa usiku (hadi 80-90%) kwa kutumia vifaa vya kutoa unyevunyevu. Dawa za kudhibiti kibaiolojia inayofahamika kama Pentaphage ina ufanisi katika kudhibiti bakteria anayesababisha ugonjwa huu. Dawa za kuzuia kuvu za shaba za kikaboni zinaweza kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa.
Daima zingatia njia jumuishi pamoja na hatua za kinga na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Dawa za kuua wadudu zenye shaba hidroksidi (copper hydroxide) zinaweza kutumika. Matibabu haya yana ufanisi zaidi wakati joto liko juu ya 24 °C na majani yana unyevunyevu. Kupulizia dawa wakati wa joto kali na majani yakiwa makavu kunaweza kudhuru mimea. Kupulizia dawa kila wiki inaweza kuwa muhimu ili kufikia udhibiti wa ugonjwa.
Dalili husababishwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama Pseudomonas syringae, ambao wanaweza kuambukiza mimea yote ya jamii ya matango. Bakteria hawa huishi kwenye mbegu zilizoathirika au kwenye mabaki ya mimea kwenye udongo kwa zaidi ya miaka 2. Wakati unyevu unapokuwa juu, tone la ute unaonata la bakteria, lenye mwonekano angavu hadi mweupe hutokea kwenye maeneo yaliyoambukizwa. Bakteria hawa husafiri kutoka mmea mmoja hadi mwingine kwa njia ya mikono na vifaa vya kazi za shambani vya wafanyakazi, kwa njia ya wadudu, au kwa rasharasha za maji au upepo. Hatimaye, bakteria huingia kwenye mmea kupitia vinyweleo (vitundu vidogo sana) vilivyo kwenye uso wa jani (stomata). Wakati matunda yanapoambukizwa, bakteria huzamia ndani ya nyama ya tunda na kuathiri mbegu. Cha kushangaza, maambukizi ya majani kwa virusi vinavyosababisha kufa kwa tishu za majani ya tumbaku hutoa kiwango fulani cha kinga dhidi ya bakteria wanaosababisha Ugonjwa wa Doa Pembe la majani.