Xanthomonas sp.
Bakteria
Dalili za awali ni vidonda vidogo, vya kijani-njano kwenye majani machanga, ambayo kwa kawaida huonekana yakiwa yameharibika umbo na kujisokota. Juu ya majani ya zamani, vidonda vina pembe, kijani kibichi, na vina mafuta (grisi) kwa kuonekana, mara nyingi huzungukwa na miduara ya njano. Mara nyingi huwa vingi zaidi kwenye kingo za majani au ncha. Hatimaye, madoa huonekana kama matundu kwa sababu katikati hukauka na kusambaratika. Madoa ya matunda (hadi sm 0.5) huanza kama maeneo ya kijani mpauko, yaliyotota maji, ambayo hatimaye huwa na mikwaruzo, kuwa kahawia na yenye magaga.
Doa Bakteria ni ngumu sana na ni ghali kutibu. Ikiwa ugonjwa utatokea mapema kwenye msimu, fikiria kuharibu mazao yote. Dawa za bakteria zilizo na shaba huweka utando wa kinga kwenye majani na matunda. Virusi vya bakteria (bacteriophages) ambavyo vinaua bakteria vinapatikana. Loweka mbegu kwa dakika moja kwenye sodium hypochlorite 1.3% au kwenye maji moto (50°C) kwa dakika 25.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua bakteria zenye shaba zinaweza kutumika kama kinga na kutoa udhibiti wa ugonjwa kwa kiasi kidogo. Tumia dawa pale ishara ya kwanza ya ugonjwa ikitokea na kisha kwa vipindi vya siku 10 hadi 14 wakati hali ya joto na unyevu inapotawala. Viambata hai vya shaba na mancozeb hutoa ulinzi bora.
Doa bakteria hutokea duniani kote na ni mojawapo ya magonjwa mabaya zaidi kwenye mimea ya pilipili na nyanya inayokuzwa katika mazingira ya joto na unyevu. Vimelea vinaweza kuishi kwa kuambatana na mbegu, ama nje au ndani na pia kwenye magugu maalum na baadaye kuenea kwa njia ya mvua au umwagiliaji wa juu. Huingia kwenye mmea kupitia vitundu vya majani na majeraha. Joto bora zaidi kwao huanzia 25 hadi 30 ° C. Mara baada ya mazao kuambukizwa, ugonjwa ni vigumu sana kudhibiti na unaweza kusababisha hasara ya jumla ya mazao.