Mahindi

Doa Laini la Jani

Pseudomonas syringae pv. syringae

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Ubadilikaji wa rangi ya kijani ang'avu inayopitisha mwanga hutokea sambamba na vishipajani vya majani ya chini.
  • Vidonda hivi hutanuka kwa urefu na huwa na tabia ya kuungana.
  • Mistari ya kahawia inayotokana kufa kwa tishu katikati yake hukauka na kudondoka, na kufanya jani lionekane limechanika.
  • Wakati mwingine ute au mchuruziko wa bakteria huonekana kwenye tishu zenye maambukizi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mahindi

Dalili

Mwanzoni vidonda hutokea vya rangi ya kijani ang'avu hadi ya mzeituni (Kijani ya manjano yenye giza) inayopitisha mwanga vinavyoenda sambamba na vishipajani vya majani ya chini. Polepole, vidonda hivi huanza kuonekana pia kwenye majani ya juu. Katika hali muafaka za hewa, vidonda hivi huongezeka kwa urefu na kupelekea kuungana. Ute (mchuruziko) wa bakteria wakati mwingine huonekana kwenye tishu zilizoathirika katika hatua za mwanzo za ugonjwa. Kadri mimea inavyozeeka, vidonda hivi hutengeneza mistari ya kahawia (kutokana na kufa tishu za majani) katikati ya majani, ambayo baadaye hukauka na kudondoka, na kufanya jani lionekane limechanika. Kwa baadhi ya aina za mahindi zinazoweza kuathirika, inaweza kuonekana mistari ya njano kwenye majani yaliyojisokota na kubadilika umbo la vifundo vya juu vya mmea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi sasa, hakuna matibabu ya asili (bila kutumia dawa za kemikali) yenye ufanisi yanayopatikana. Njia mbadala za kudhibiti doa bakteria kwenye mahindi zinaishia tu kwenye matumizi ya hatua za kuzuia na mbinu bora za kilimo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima panga mbinu jumuishi za usimamizi wa mimea dhidi ya wadudu au magonjwa, ikiwa ni pamoja na hatua za kukinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Kwa sasa, matibabu ya kemikali yanategemea bidhaa za shaba au zile zilizochanganywa na shaba. Upuliziaji mara nyingi una ufanisi wa kiwango kidogo tu, na hivyo kufanya ugonjwa huu kuwa mgumu sana kuudhibiti mara ugonjwa unapojitokeza.

Ni nini kilisababisha?

Dalili za ugonjwa huu hutegemea sana nguvu ya vimelea, aina ya mahindi, na hali ya mazingira. Bakteria huyu huishi kwenye mabaki ya mazao kwenye udongo, kwenye mimea mbadala inayohifadhi vimelea vya bakteria huyu, magugu, na mimea inayoota yenyewe. Bakteria husambazwa kwenye mimea mbalimbali kwa njia ya maji ya umwagiliaji, upepo, au wafanyakazi na vifaa vya kilimo vilivyochafuliwa na bakteria. Aidha, bakteria hawa huingia ndani ya mmea kupitia matundu ya asili au majeraha. Vilevile wanaweza kuhimili joto la kati ya 0 na 35°C, lakini hustawi zaidi kwenye halijoto ya kati ya 25-30°C. Ugonjwa huu huwa mbaya zaidi wakati wa vipindi vya hali ya hewa yenye unyevu wa majimaji. Ikiwa ugonjwa unajitokeza mapema katika msimu, baadhi ya wakulima huchagua kuharibu mazao yote kwa kuyachimbua.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu kutoka kwa mimea yenye afya au vyanzo vilivyothibitishwa.
  • Chagua aina za mbegu zinazostahimili magonjwa ambazo zinapatikana kwenye soko lako.
  • Panda kwa kuchelewa ili kuepuka hali ya hewa yenye maji maji inayowezesha kusambaa kwa ugonjwa.
  • Epuka kufanya kazi shambani wakati majani yamelowana.
  • Epuka umwagiliaji wa kutokea juu.
  • Safisha shamba kwa kuondoa magugu na mimea mbadala inayoweza kuhifadhi vimelea vya magonjwa.
  • Usiozeshe (na kuwa mboji) au kuacha mabaki ya mimea karibu na mashamba.
  • Takasa (safisha) zana zako za kilimo kwa kutumia pombe kali au moto (si vyote).
  • Ondoa mara moja mimea iliyoambukizwa na choma mabaki yake.
  • Inashauriwa kufanya mzunguko wa mazao kwa kutumia mazao yasiyoathirika na ugonjwa huu.

Pakua Plantix