CiYMV
Kirusi
Dalili huanza kama madoa madogo ya njano kwenye majani mapya, ambayo baadaye huwa makubwa na kutengeneza michoro ya njano angavu sambamba na mishipa ya jani. Majani yaliyokomaa yanakuwa na mwonekano au mguso wa mithili ya ngozi na majani machanga hubaki kuwa madogo. Matunda huonesha madoa ya manjano na maeneo ya kijani yaliyoinuka. Ukuaji wa mti na uzalishaji wa matunda huathirika.
Udhibiti hai/asilia hauwezekani kwa tatizo hili.
Udhibiti kwa kutumia madawa ya kemikali kwa wadudu wanaosambaza kirusi hiki hautoshi kudhibiti virusi. Hakikisha wakati wote unatumia vipandikizi visivyo na virusi.
Virusi wa Njano wa Mozaiki wa Michungwa(CYMV), maarufu kama Batobato ya Michungwa waligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini India na kwa sasa ni wa kawaida huko Andhra Pradesh, India, ambako mimea jamii ya michungwa hulimwa kwa kiwango kikubwa. Ugonjwa huu unaweza kusambaa kupitia vipandikizi vilivyoathiriwa na vitalu vingi vya uzalishaji wa kibiashara vimeripoti matukio ya ugonjwa huu. Virusi pia vinaweza kusambazwa na kidung'ata wa michungwa na kupitia zana zilizochafuliwa. Virusi vinaweza kusambaa kutoka mti mmoja hadi mingine kupitia dodder, ambayo ni magugu ya kawaida.