Kiazi

Virusi vya mop-top

PMTV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Madoa ya manjano angavu na mifumo ya miduara kwenye majani ya chini au ya kati.
  • Miundo ya nkshi kwenye majani ya juu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Kiazi

Dalili

Kwenye mashina, mifumo bainifu hukua na madoa ya manjano angavu na miduara au miundo ya mstari kwenye majani ya chini au ya kati. Dalili isiyo ya kawaida ni kuwepo kwa muundo wa rangi ya njano uliofifia, wenye umbo la V kwenye vipande vya majani machanga ya juu na kusababisha muundo wa nakshi tofauti. Mop-top husababisha ufupishaji mkubwa wa pingili za mashina unaoambatana na msongamano au mrundikano wa majani. Baadhi ya majani madogo yanaweza kuwa na kingo za mawimbi au kuviringishwa na kusababisha ukuaji duni na ulioshikana. Miduara yenye kipenyo cha 1 - 5 cm iko kwenye uso wa tunguu. Viazi vinaweza pia kuwa na mistari ya kahawia yenye tishu zilizokufa, miinuko na miduara kwenye mwili.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Fuatilia uwepo wa virusi kwa kutenganisha virusi kwa kutumia udongo na njia ya mimea ya chambo na ufanyie uchunguzi wa mapema kwa kutumia mimea ya viashiria. Panda aina za viazi ambazo hazionyeshi dalili za kufa kwa tishu za kiazi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu iliyo jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu yanayopatikana ya kibaolojia. Hakuna udhibiti wa kemikali wenye ufanisi na salama kwa mazingira wa ugonjwa huu na njia bora ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo ni kupanda viazi visivyo na virusi kwenye ardhi isiyo na PMTV.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu huo unasababishwa na virusi vya mop-top vya viazi (PMTV), ambavyo huishi kwenye udongo ndani ya vijimbegu bwete vya kuvu mwenezaji wake. Kuvu wa upele wa unga (Spongospora subterranea) ni kiumbe kinachoenezwa na udongo na ndiye msambazaji pekee wa virusi hivi. Virusi pia vinaweza kuambukizwa kwa njia ya upili kupitia shughuli zinazosababisha kuhama kwa udongo na viazi pia vinaweza kuchafuliwa wakati wa kuhifadhi na kuchambua kupitia vumbi linalotoka kwenye sehemu iliyochafuliwa ya mbegu. Virusi na waenezaji wake hupatikana katika hali ya hewa ya baridi na yenye unyevunyevu. Uwepo wa ugonjwa huu unaweza kusababisha hasara kubwa ya mavuno katika aina nyeti kutokana na kupungua kwa uzalishaji na ubora wa viazi.


Hatua za Kuzuia

  • Panda tunguu za viazi visivyo na virusi kwenye udongo usio na virusi.
  • Fuatilia mashamba mara kwa mara kwa uwepo wa virusi.
  • Dumisha mazoea ya usafi kwenye mashamba.

Pakua Plantix