Bamia

Batobato ya Mishipa-jani ya Njano

BYVMV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Ugonjwa huu wa virusi wa Bamia unaweza kusababisha hasara kubwa ya mavuno.
  • Hutokea katika hatua zote za ukuaji wa mazao na huenezwa na inzi weupe (Bemisia tabaci).
  • Kutokea kwa mishipa ya njano na mifumo ya nakshi kwenye majani.
  • Mavuno ya matunda yanaweza kupunguzwa kwa kiwango cha juu hadi 96% ikiwa mazao yameambukizwa katika hatua ya awali.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Bamia

Dalili

Ugonjwa huo una sifa ya viwango tofauti vya mabadiliko ya rangi ya mishipa kuwa njanona, na vile vile madoa ya kupokezana ya kijani na njano yenye muundo wa nakshi, majani madogo, matunda machache na madogo, na ukuaji wa mimea kudumaa. Mwanzoni, majani yaliyoambukizwa yanaonyesha manjano tu ya mishipa, lakini jani lote hugeuka manjano katika hatua za baadaye. Mimea inapoambukizwa siku 20 baada ya kuota, hubakia kudumaa. Ikiwa majani machanga yataambukizwa mapema katika msimu, huwa manjano kabisa, kahawia na kisha kukauka. Mimea iliyoambukizwa baada ya maua ina sifa ya majani ya juu na sehemu za maua zinazoonyesha dalili za kuoshwa mishipa. Bado mimea itatoa matunda kadhaa lakini yanageuka manjano na kuwa magumu. Mimea ambayo ilikuwa na afya na kuzaa kawaida hadi mwishoni mwa msimu basi itapata vichipukizi vichache kwenye sehemu ya chini ya shina.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Zuia wadudu waenezao virusi kwa kunyunyizia 5% mafuta ya mbegu za mwarobaini, au tangawizi, vitunguu saumu na vimiminika vya pilipili. Kata vipande vya mmea wa kakati (cactus), au kakati penseli (bush milk), chovya ndani ya maji (ya kutosha vipande kuelea), iruhusu ichachuke kwa siku 15. Chuja na nyunyiza mimea iliyoathirika. Paka mafuta ya mwarobaini na haradali, Rhizobacteria, mafuta ya Crozophera ikifuatiwa na mafuta ya Palmarosa. Mchanganyiko wa mafuta (0.5%) na (0.5%) ya sabuni pia inaripotiwa kusaidia.

Udhibiti wa Kemikali

Virusi haviwezi kudhibitiwa kabisa kwa njia za kemikali. Kwa hiyo, inashauriwa kuzingatia kila wakati mbinu iliyojumuishwa na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia, ikiwa yanapatikana. Uwekaji wa mapema wa viua wadudu kwenye udongo dhidi ya vikundi fulani vya nzi weupe na magonjwa inaonekana kuwa njia bora zaidi. Nzi weupe hutengeneza ukinzani/usugu kwa dawa zote, kwa hivyo mzunguko wa dawa tofauti unapendekezwa. Dawa mbili za kunyunyuzia za Acetamiprid 20SP (40g a.i/ha) zimethibitishwa kuwa na ufanisi katika kupunguza matukio ya virusi vya batobato na hatimaye kuongeza mavuno ya Bamia. Imidacloprid 17.8% SL ikitumika mara mbili na matibabu ya mbegu moja (Imidacloprid @ 5 gm/kg ya mbegu) inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wadudu hadi 90.2%.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu huo husababishwa na begomovirus, ambao huenezwa na nzi weupe. Virusi hawazaliani kwenye wadudu wanaowaeneza lakini huhamishwa kwa urahisi kutoka kwenye mmea hadi mmea na inzi mweupe aliyekomaa kwa njia mbalimbali. Nzi weupe majike wana ufanisi zaidi kuliko madume katika kueneza virusi. Ugonjwa huu wa virusi huambukiza wakati wa hatua zote za ukuaji, hata hivyo, hatua inayohusika zaidi ni kutoka siku 35 hadi 50. Idadi ya inzi weupe na ukali wa virusi huathiriwa kwa kiasi kikubwa na halijoto, unyevunyevu, na kiwango cha chini cha joto cha 20-30°C. Mdudu wa pili muhimu zaidi katika kueneza ugonjwa huu ni panzi wa majani wa bamia(Amrasca devastans).


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina sugu kama Parbhani Kranti (Arka Abhay, Varsha, Uphar) na Arka Anamika.
  • Dumisha nafasi sahihi kati ya mimea.
  • Panda Mahindi au Marigold kama zao la mpakani ili kunasa wadudu waharibifu.
  • Epuka kupanda msimu wa kiangazi kwani huu ndio msimu wa kilele wa inzi weupe.
  • Epuka kupanda aina zinazoshambuliwa kirahisi katika msimu wa kiangazi, wakati nzi weupe wakiwa amilifu kwa kiasi kikubwa.
  • Weka mitego ya kunata ya manjano (12/ekari) juu ya kimo cha mmea ili kufuatilia na kukamata wadudu waenezaji.
  • Kuharibu magugu na mimea mwitu mingine, hasa Croton sparsiflora na Ageralium spp., wakati wowote iwezekanavyo.
  • Ondoa mimea iliyoathirika kutoka shambani na uichome moto.

Pakua Plantix