AMV
Kirusi
Madoa ya manjano yanayong'aa au madoa ya mozaiki yanakua kwenye majani, na hivyo kusababisha kubadilika kwa rangi kuwa ya shaba nyeusi. Pete/miduara ya seli zilizo kufa na madoa hukua kwenye matunda. Tishu ya phloem, pamoja na phloem kwenye mizizi, zinakuwa na seli zilizo kufa na kusababisha kifo cha mmea.
Tumia matandazo ya rangi ya fedha yanayo akisi mwanga ili kuchelewesha kuambukizwa na virusi vinavyoenezwa na vidukari na kupunguza matukio na ukali wa magonjwa haya kwa kuwafukuza vidukari wanao waambukiza. Weka matandazo ya polyethilini ya kuakisi kwenye vitanda vya kupandia kabla ya kuotesha au kupandikiza ili kupunguza kutua kwa vidukari na maambukizi ya virusi.
Daima zingatia mbinu iliyo jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia yanayopatikana. Hakuna mikakati madhubuti ya udhibiti wa kemikali inayopatikana kwa sasa. Viua wadudu vinavyolenga kudhibiti vidukari havifanyi kazi.
Uharibifu husababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbegu, ambavyo huishi katika mbegu zilizoambukizwa au mimea inayohifadhi wadudu hao. Maambukizi ya upili yanaweza kutokea wakati vidukari wakieneza virusi kutoka kwa mbegu za mimea iliyoambukizwa hadi mimea yenye afya kwa njia isiyo na mwendelezo. Mara tu vidukari wanapopata virusi, huwa na uwezo wa kusambaza virusi kwa muda mfupi tu na ueneaji ni wa haraka na wa ndani ya eneo dogo.