CLCuV
Kirusi
Dalili kuu za virusi vya kupindisha majani ya pamba ni upindaji wa majani kuelekea juu. Zaidi ya hayo, mishipa ya majani inaweza kuongezeka unene na kuwa na rangi ya giza, na vichipukizi vinaweza kutokea upande wa chini wa majani, kwa kawaida vikiwa na umbo la majani. Maua yanaweza kubaki yamejifunga na kisha kudondoka pamoja na vitumba vya pamba. Ikiwa mimea itaambukizwa mapema katika msimu, ukuaji wake utadumaa na mavuno yatapungua kwa kiasi kikubwa.
Idadi ya nzi weupe kwa ujumla inaweza kudhibitiwa na maadui wa asili (kama vile mbawakimia, wadudu wa macho makubwa, wadudu haramia), hivyo kuwa makini usiue wadudu hawa kwa kupuliza dawa za kuua wadudu bila mpangilio. Mafuta ya mwarobaini au mafuta yanayotokana na petroli yanaweza kutumika na yanapaswa kufunika/kuenea kwenye mimea vizuri, hasa upande wa chini wa majani. Utafiti wa hivi karibuni pia umeonyesha uwezekano wa kutumia vijidudu vya udhibiti wa kibaolojia kama vile uzao wa bakteria wenye manufaa (k.m. Bacillus, Pseudomonas, na Burkholderia) kama njia ya kupunguza uwepo wa virusi.
Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia endapo yanapatikana. Hakuna njia zozote zinazojulikana za kuzuia au kupunguza virusi vya kupinda majani ya pamba. Udhibiti wa kemikali kwa kutumia dawa za kuua wadudu unaweza kutumika kudhibiti idadi ya nzi weupe, kama vile imidacloprid au dinotefuran. Hata hivyo, dawa za kuua wadudu zinapaswa kutumika kwa uangalifu, kwa sababu matumizi kupita kiasi ya dawa hizi yamefanya spishi nyingi za nzi weupe kuwa sugu dhidi ya dawa hizi. Ili kupunguza uwezekano wa jambo hili kutokea, hakikisha unabadilisha dawa za kuua wadudu unazotumia.
Dalili zinasababishwa na virusi vya kukunja majani ya pamba, ambavyo kimsingi husambazwa kupitia nzi weupe. Kuenea kwa ugonjwa huu kwa kiasi fulani kunategemea upepo unaotoka na kuelekea upande mmoja, na hivyo utaonyesha umbali kiasi gani nzi hawa wanaweza kusafiri. Nzi weupe ni tatizo kubwa zaidi katikati ya msimu hadi mwishoni mwa msimu. Ugonjwa huu pia unahusishwa na makazi, kama vile miti. Kwa kuwa ugonjwa huu hausambazwi na mbegu, virusi vinaendelea kuwepo katika mazingira kupitia mimea mbadala (kama vile tumbaku na nyanya) na magugu yanayoweza kuhifadhi nzi hawa au vimelea vyake. Sababu zingine zinazoweza kusaidia ukuaji wa ugonjwa huu ni mvua za hivi karibuni, miche iliyoathiriwa, na uwepo wa magugu. Virusi pia vina uwezekano mkubwa wa kuenea katika hali ya joto la kati ya 25-30ºC. Katika vitalu, mimea ya pamba inakuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa wakati ipo katika hatua za miche na ukuaji.