CMV
Kirusi
Dalili hutofautiana sana kulingana na aina iliyoambukizwa na hali za kimazingira. Katika baadhi ya matukio, virusi vinaweza kuwepo lakini dalili hufichwa au kutoonekana kirahisi. Katika aina zinazoshambuliwa, mabaka ya rangi ya njano au rangi ya kijani nyepesi na madoa ya njano yanaweza kuonekana kwenye majani na matunda. Katika aina fulani, muundo wa wazi wa doa la mduara au mstari wa tishu zilizo kufa unaweza kuonekana. Majani machanga yanaonekana yamekunjamana na membamba na majani ni ya kijani kilicho pauka/fifia na yenye mwonekano wa ngozi. Mmea wote hudumaa kwa kiasi kikubwa na umbo lililo haribiwa, wenye muonekano wa kichaka, na mara nyingi hauzai. Ikiwa yatakuepo, matunda yana vidonda vingi vya mviringo vya kahawia, mara chache huwa na mduara angavu wa njano.
Matumizi ya dawa za kunyunyuzia za mafuta ya madini kwenye majani yanaweza kuzuia vidukari kula na hivyo kudhibiti idadi yao.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna kemikali zinazofaa dhidi ya CMV, wala yoyote ambayo hulinda mimea kutokana na kuambukizwa. Viua wadudu vyenye cypermethrin au chlorpyrifos vinaweza kutumika kama dawa ya majani dhidi ya vidukari.
Dalili husababishwa na virusi vya matango (CMV), ambavyo huathiri aina mbalimbali (mazao pamoja na maua mengi, hasa maua ya lily, delphiniums, primulas na daphnes). Virusi vinaweza kubebwa na kusambazwa na spishi 60-80 tofauti za vidukari. Njia zingine za maambukizi ni pamoja na mbegu zilizoambukizwa na vipandikizi, na uhamisho wa kupitia kwenye mikono ya mfanyakazi au kwenye zana. CMV inaweza kuishi msimu wote wa baridi katika magugu ya kudumu ya maua, na mara nyingi pia juu ya mazao yenyewe, katika mizizi, mbegu au maua. Katika maambukizi ya awali, virusi hukua kimfumo ndani ya mche mpya na kuishia kwenye majani ya juu. Vidukari wakila mimea hii hubeba virusi kwenda kwenye mimea mingine (maambukizi ya upili). Virusi hutumia tishu za mishipa ya mimea kwa usafiri wa umbali mrefu kati ya viungo tofauti vya mmea.