CLCV
Kirusi
Dalili za virusi vya mkunjo wa Jani la pilipili ni kingo za majani kupinda/kujikunja kuelekea juu, mishipa ya njano na kupungua kwa ukubwa wa jani. Zaidi ya hayo, mishipa ya majani huvimba na kupungua kwa urefu wa pingili na vikonyo. Majani ya zamani huwa kama ngozi na kukakamaa. Ikiwa mimea imeambukizwa mwanzoni mwa msimu, ukuaji wake utadumaa, na kusababisha upungufu mkubwa wa mavuno. Uzaaji wa matunda katika mimea inayoshambuliwa kirahisi haukamiliki na matunda yaliyo haribika umbo. Virusi husababisha dalili zinazofanana na uharibifu unatokana na ulaji wa vithiripi na utitiri.
Dhibiti idadi ya nzi weupe ili kupunguza maambukizi ya virusi. Mafuta ya mwarobaini au mafuta ya mazao ya bustani (mafuta yanayotokana na petroli) yanaweza kutumika. Hakikisha kwamba mafuta yanafunika mimea vizuri, hasa upande wa chini wa majani ambapo inzi weupe wanaweza kupatikana. Baadhi ya maadui wa asili kama vile mbawakimia, kunguni wenye macho makubwa na mende haramia wadogo wanaweza kudhibiti idadi ya inzi weupe.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Hakuna njia madhubuti zinazojulikana za kuzuia au kupunguza virusi vya mkunjo wa jani la pilipili. Fuata mbinu za kudhibiti kemikali, kama vile imidacloprid au dinotefuran. Nyunyizia miche kwa imidacloprid au lambda-cyhalothrin kabla ya kuipandikiza ili kudhibiti wadudu wanaoeneza. Matumizi makubwa ya viua wadudu hudhuru wadudu wenye manufaa na pia kufanya spishi nyingi za nzi weupe kuwa sugu. Ili kuzuia hili, hakikisha mzunguko sahihi kati ya viua wadudu na utumie tu vile vilivyo chaguliwa.
Dalili husababishwa na begomovirus, ambao kimsingi huenezwa na nzi weupe kwa njia inayoendelea. Wana sifa ya urefu wa 1.5 mm, mbawa nyeupe zinazo nata, mwili wa njano hafifu na hupatikana mara kwa mara kwenye upande wa chini wa majani. Kuenea kwa ugonjwa hutegemea hali ya upepo, ambayo huamua ni umbali gani nzi weupe wanaweza kusafiri. Nzi weupe huleta matatizo zaidi katikati ya msimu au mwishoni. Kwa kuwa ugonjwa huu hauenezwi kwa mbegu, virusi huendelea kuwepo katika mazingira kupitia mimea mbadala (kama vile tumbaku na nyanya) na magugu. Baadhi ya mambo ya ziada ambayo yanaweza kuchangia ukuaji wa ugonjwa huo ni mvua, vipandikizi vilivyo ambukizwa, na uwepo wa magugu. Katika vitalu, mimea ya pilipili huathiriwa zaidi na maambukizi wakati wa miche na hatua ya kuchipua.