Pamba

Kirusi wa Mchirizi ya Tumbaku

TSV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Mabaka makubwa ya manjano au ya kahawia kwenye majani yanayounda muundo wa mozaiki/nakshi na tishu za kijani kibichi.
  • Vishipa jani (Mishipa ya majani) vyenye rangi ya manjano, vinene na vilivyoharibika umbo.
  • Kudumaa kwa mimea, maua machache, kudondoka kwa vitumba, na kupungua kwa matawi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Pamba

Dalili

Mwanzoni, mimea iliyoathirika huwa na maeneo madogo yenye rangi ya manjano na yasiyo na umbo maalumu au ubadilikaji wa rangi kwenye majani, yanayoanzia kipenyo cha milimeta 2-5. Kadri muda unavyosonga, maeneo haya yanakuwa makubwa, yenye rangi ya manjano na umbo pembe au mabaka yanayotokana na kufa kwa tishu (rangi kubadilika kutoka manjano hadi kahawia) huku yakiwa na kipenyo kinachoanzia milimeta 5-15, ambayo huonekana kama nakshi isiyo ya kawaida ya mozaiki kwenye majani. Majani hukauka kutokana na kufa kwa tishu na yanaweza kuanguka mapema kabla ya wakati, na kusababisha kupungua kwa shazi la majani na kudumaa kwa mimea. Maua yanakuwa machache na vitumba vinaweza pia kuanguka mapema, na hivyo kupunguza mavuno kwa kiasi kikubwa. Mishipa ya majani yaliyoathirika inakuwa ya manjano, minene na iliyopindika. Dalili hizi huonekana mara nyingi kwenye majani machanga ambayo huonekana kuwa na rangi iliyofifia zaidi kuliko majani yenye afya, mara nyingi yakiwa na ncha zilizodumaa kukua. Sehemu zilizoathirika shambani kwa ujumla huonekana kuwa na rangi iliyofifia.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna tiba ya moja kwa moja ya kibaiolojia dhidi ya kirusi michirizi cha tumbaku. Hata hivyo, kuna chaguzi nyingi za kudhibiti wadudu wanaobeba virusi wake, vidukari na vithiripi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi hayawezekani, lakini wadudu wanaobeba magonjwa kama vile vithiripi, vidukari, na wadudu wengine wanaofyonza wanaweza kudhibitiwa kwa kiwango fulani. Kagua kanzidata (hifadhidata) kuangalia matibabu ya kikemikali dhidi ya vithiripi na vidukari kwa maelezo zaidi, kwa mfano fipronil (2 ml/l) au thiamethoxam (0.2 g/l).

Ni nini kilisababisha?

Dalili za ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoweza kuishi kwenye mimea kadhaa mbadala, na miongoni mwa mimea hiyo ni tumbaku ( na hivyo kutoa jina la ugonjwa), asparaga, stroberi, soya, na alizeti. Kwa kuwa virusi vinaweza kuenezwa kwa njia ya mbegu, chanzo kikuu cha maambukizi kinaweza kuwa mbegu zilizoathirika. Usambazaji wa pili kutoka mmea mmoja hadi mwingine unafanyika kupitia wadudu/vijidudu vinavyobeba magonjwa (kama vile vidukari au vithiripi) au kupitia majeraha ya mimea yanayotokana na kazi za shamba. Dalili na athari kwenye mavuno zinategemea aina ya mmea, hali ya mazingira (joto na unyevu), na hatua ya ukuaji ambayo mmea uliathirika. Kwa kawaida maambukizi ya kuchelewa yanayotokana na vidukari huwa na athari ndogo kulinganisha na maambukizi yanayosambazwa na mbegu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya kutoka vyanzo vya kuaminika.
  • Dumisha hatua kali za usafi kwa zana zote za kilimo zinazohusika kwenye ulimaji wa pamba.
  • Kagua mimea yako au shamba lako ili kugundua dalili zozote za ugonjwa na vijidudu vinavyobeba magonjwa kama vile vidukari na vithiripi.
  • Ondoa kwenye mashamba mimea iliyoathirika na mabaki ya mimea, na iharibu kwa kuizika ardhini au kuichoma.
  • Usisambaze machipukizi kutoka shamba moja hadi lingine.
  • Epuka kupanda mimea mbadala inayohifadhi virusi vya michirizi ya tumbaku kama vile asparaga, stroberi, soya, alizeti, mboga ya saladi, na tumbaku karibu na shamba la pamba.

Pakua Plantix