CMD
Kirusi
Michoro ya mozaiki/nakshi au madoa kwenye majani hujitokeza katika hatua za awali za ukuaji wa majani. Mabadiliko ya rangi huonekana kama maeneo ya manjano hafifu au karibu na nyeupe miongoni mwa sehemu zilizobaki za kijani. Muundo wa mozaiki/nakshi unaweza kusambaa sawasawa kwenye jani zima au kuonekana kwenye maeneo machache, mara nyingi kwenye sehemu kitako cha jani. Majani yenye maumbo yaliyo haribika, kupotoka, na kupungua kwa ukubwa wa vipande vya majani vinaweza kuonekana katika maambukizi makali. Baadhi ya vipande vya majani vinaweza kuonekana vya kawaida au kuonekana kana kwamba vinaanza kupona, kulingana na halijoto ya mazingira na ustahimilivu wa mmea. Hata hivyo, dalili zinaweza kujirudia ikiwa kuna hali nzuri za kimazingira kwa virusi. Kupungua kwa uzalishaji wa majani huathiri ukuaji wa jumla wa mmea na uzalishaji wa mihogo. Ukubwa wa mhogo unategemea moja kwa moja ukali wa maambukizi, ambapo mimea iliyoathirika sana haina mihogo kabisa.
Hakuna hatua za kudhibiti virusi kwa njia ya kibaolojia zinazopatikana. Hata hivyo, nzi mweupe ana maadui wengi na wadudu wanaoweza kutumika kama wadhibiti wa kibiolojia. Udhibiti wa kibaolojia unaowezekana unajumuisha spishi mbili za jenasi Isaria (zamani Paecilomyces), zikiwa na spishi mbili Isaria farinosa na Isaria fumosorosea.
Kila wakati zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanapatikana. Viambato amilifu ambavyo vimeripotiwa kuwa na athari katika kudhibiti idadi ya nzi weupe duniani kote ni pamoja na bifenthrin, buprofezin, fenoxycarb, deltamethrin, azidirachtin na pymetrozine. Hata hivyo, tumia bidhaa hizi kwa uangalifu, kwani matumizi yasiyo ya busara mara nyingi husababisha kuongezeka kwa ukinzani kwa wadudu.
Dalili za ugonjwa wa virusi vya mozaiki ya mihogo husababishwa na kundi la virusi ambavyo mara nyingi huambukiza mimea ya mihogo kwa pamoja. Virusi hivi vinaweza kuenezwa kwa muda mrefu na nzi mweupe aina ya Bemisia tabaci pamoja na vipandikizi vilivyotokana na mimea iliyoambukizwa. Nzi weupe husafirishwa na upepo unaovuma na wanaweza kusambaza virusi kwa umbali wa kilomita kadhaa. Aina za mihogo zinatofautiana sana katika uwezekano wa kuathiriwa na virusi, lakini kwa ujumla, majani machanga ndiyo yanayoonyesha dalili za kwanza, kwani nzi weupe hupendelea kula tishu changa na laini. Usambazaji wa virusi hutegemea sana idadi ya mdudu huyu, ambaye pia huathiriwa na hali ya hewa iliyopo. Ikiwa idadi kubwa ya nzi weupe itaambatana na ukuaji mzuri wa mihogo, virusi vitaenea haraka. Joto linalopendelewa na mdudu huyu linakadiriwa kuwa kati ya nyuzi 20°C hadi 32°C.