Ndizi

Batobato ya Tango Kwenye Mgomba

CMV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Muundo wa madoa ya kijani iliyofifia na kijani kibichi na nakshi kwenye majani.
  • Matunda yaliyoathirika yanaweza kuonekana madogo na yanaweza kuonyesha mistari ya manjano au kufa kwa tishu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Ndizi

Dalili

Maambukizi yanaweza kutokea katika hatua yoyote ya ukuaji wa mti na huonekana zaidi kwenye majani. Dalili za awali ni mitindo mithili ya nakshi inayoendelea au iliyokatika sambamba na vishipajani (mishipa ya majani). Majani yanaweza kupata muonekano kama yameabanduliwa. Baada ya muda, uso wa jani, yaani lamina haukui kikamilifu na kingo huonekana umepinda isivyo kawaida na unaweza kuonesha madoa yanayotokana na kufa kwa tishu. Majani machanga vile vile yanaweza kupungua ukubwa wake. Maeneo yaliyooza yanaweza kuonekana kwenye ala/kifuko-jani na kuenea zaidi hadi kwenye shina bandia na tunguu. Majani ya zamani huonesha dalili za ufaji wa tishu kama mistari ya rangi nyeusi au zambarau na hudondoka. Mimea iliyoathirika haiwezi kukomaa na inaweza kushindwa kutoa mikungu. Matunda hayaoneshi dalili mara zote lakini mara nyingi huonekana kuwa madogo na yanakuwa na mistari ya manjano au kufa kwa tishu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi hayawezekani, lakini inawezekana kupunguza hatari ya maambukizi kupitia vidukari. Kuna maadui mbalimbali wa asili wanaoweza kutumika kwa ufanisi dhidi ya spishi za vidukari kama vile wadudu wa vimelea, wadudu wanaokula wadudu wengine, na spishi za kuvu. Matibabu ya joto kavu ya machipukizi ya mizizi kwa nyuzijoto 40°C kwa siku moja inaweza pia kusaidia kupunguza hatari ya maambukizi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi hayawezekani, lakini mimea mbadala inayohifadhi magonjwa(bila yenyewe kuonesha dalili) na wadudu wanaobeba vimelea vya magonjwa vinaweza kudhibitiwa kwa kiwango fulani. Ikiwa viuatilifu vinahitajika, bidhaa zenye demeton-methyl, dimethoat, na malathion zinaweza kutumika kama dawa za kunyunyizia kwenye majani. Tafadhali kumbuka kuwa kemikali zilizoorodheshwa zina athari zenye sumu hadi sumu kali kwa afya ya binadamu na pia kwa wanyama.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na virusi. Maambukizi ya awali hutokea kupitia mbegu zilizoathirika kama vile machipukizi ya mizizi yanayotumika kama miche. Spishi za vidukari hutumika kama wasambazaji wa maambukizi ya upili na kusambaza chembe chembe za virusi kwa mimea au mashamba mengine. Tango na nyanya ni mimea inayohifadhi virusi, yaani, inaweza kuhifadhi chembe za virusi bila kuonyesha dalili zozote. Maambukizi hupendelea hali maalum za hewa kama vile mvua za mara kwa mara, kwa mfano, wakati wa mwishoni na baada ya msimu wa mvua. Ugonjwa huu ni tishio kubwa kwa mimea ya migomba na unaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mavuno.


Hatua za Kuzuia

  • Tekeleza hatua kali za karantini ikiwa zipo.
  • Tumia vifaa vya kupanda (kv mbegu, miche, machipukizi) vilivyo na afya kutoka vyanzo vya kuaminika.
  • Usipande aina za mimea inayoweza kuathiriwa kirahisi ndani ya shamba.
  • Kagua mara kwa mara mimea yako au shamba lako ili kugundua dalili zozote za ugonjwa na wachukuzi kama vile vidukari.
  • Usilime mimea mbadala inayoweza kuhifadhi ugonjwa huu kama vile mimea ya familia ya nyanya na tango, mahindi, na spishi za jenasi za Panicum na Digitalia karibu na mashamba ya migomba.
  • Panda mimea kizuizi kama vile brown hemp (Crotalaria juncea) katika mistari mitatu kati ya minne ili kufuatilia vidukari wanaoingia kutoka mashamba yaliyoathirika.
  • Ondoa mimea iliyoathirika kutoka shambani, na iharibu kwa kuchimbia chini au kuichoma moto.
  • Usisambaze machipukizi kati ya mashamba tofauti.

Pakua Plantix