TMV
Kirusi
Sehemu zote za mmea zinaweza kuathirika katika hatua yoyote ya ukuaji. Dalili zinategemea hali za kimazingira (mwangaza, urefu wa siku, joto). Majani yaliyoambukizwa yanaonyesha madoa ya kijani na njano au muundo wa nakshi. Majani machanga yanaweza kuharibika umbile kwa kiwango kidogo. Majani ya zamani huonesha maeneo ya kijani kibichi yaliyoinuka. Katika hali fulani, mistari ya myeusi inayotokana na kufa kwa tishu inaweza kuonekana kwenye mashina na vikonyo. Mimea hudumaa kwa viwango tofauti na na utokeaji wa matunda unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Uivaji wa matunda ambapo tunda huiva sehemu moja kwanza kabla ya nyingine husababisha kutokea kwa madoa ya kahawia kwenye uso wa matunda, na ndani, madoa ya kahawia kwenye ukuta wa matunda. Mavuno yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
Zikaushe mbegu kwa joto la 70°C kwa siku 4 au kwa joto la 82-85°C kwa saa 24 kutasaidia kuondoa virusi. Vinginevyo, mbegu zinaweza kuingizwa kwa dakika 15 kwenye mchanganyiko wa 100 g/l ya fosfati ya trisodium, kisha kuzisuuza vizuri kwa maji na kisha kuzianika.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali yenye ufanisi dhidi ya Batobaro ya nyanya.
Virusi vinaweza kudumu kwenye mabaki ya mimea au mizizi katika udongo mkavu kwa zaidi ya miaka 2 (mwezi mmoja katika udongo wa aina nyingi). Mimea huambukizwa kupitia vidonda vidogo kwenye mizizi. Virusi vinaweza kusambazwa kupitia mbegu zilizoambukizwa, miche, magugu, na sehemu za mimea zenye virusi. Upepo, mvua, panzi, wanyama wadogo, na ndege, vyote hivyo vinaweza pia kubeba virusi kutoka shamba moja hadi lingine. Mbinu mbaya za kilimo wakati wa kushughulikia mimea pia zinaongeza uwezekano wa kusambaza virusi. Urefu wa siku, joto, na mwangaza, pamoja na aina ya mmea na umri wake, hutofautisha ukali wa maambukizi.