Nyanya

Virusi wa Njano Wakunja Majani ya Nyanya

TYLCV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Majani ya manjano na yaliyo kunjwa.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Idadi ndogo ya matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Nyanya

Dalili

Maambukizi katika hatua ya miche husababisha kudumaa sana kwa majani machanga na machipukizi, na hivyo kusababisha ukuaji wa muundo wa kichaka wa mmea. Katika mimea mikongwe, maambukizi husababisha matawi mengi, majani manene na yaliyokunjamana, na kubadilika rangi kwa manjano kati ya mishipa kunako onekana wazi kwenye ubapa wa jani. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huu, mimea huchukua muundo wa ngozi na kingo zilizobadilika rangi zilizo virigwa kuelekea juu na ndani. Ikiwa maambukizi yatatokea kabla ya hatua ya maua, idadi ya matunda hupunguzwa sana, ingawa hakuna dalili zinazoonekana kwenye uso wa matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu dhidi ya TYLCV. Dhibiti idadi ya nzi weupe ili kuepuka maambukizi ya virusi.

Udhibiti wa Kemikali

Mara baada ya kuambukizwa na virusi, hakuna matibabu dhidi ya maambukizi. Dhibiti idadi ya nzi weupe ili kuepuka kuambukizwa ya virusi. Viuwa wadudu vya familia ya pyrethroids vinazotumiwa kama vimiminika vya udongo au kunyunyuzia wakati wa miche vinaweza kupunguza idadi ya nzi weupe. Hata hivyo, matumizi yake kupita kiasi yanaweza kukuza upinzani katika makundi ya nzi weupe.

Ni nini kilisababisha?

TYLCV hawaenezwi kwa mbegu na hawasambazwi kimakanika. Huenezwa na nzi weupe wa spishi ya tabaci ya Bemisia. Nzi weupe hawa hula kwenye sehemu ya chini ya majani ya mimea kadhaa na huvutiwa na mimea michanga laini. Mzunguko mzima wa maambukizi unaweza kufanyika katika muda wa saa 24 na unapelekewa na hali ya hewa kavu yenye joto la juu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina sugu au zinazostahimili.
  • Panda mapema ili kuepuka idadi kubwa ya nzi weupe.
  • Panda mseto kwa safu za mimea isiyoshambuliwa kama vile maboga na matango.
  • Tumia vyandarua kufunika vitalu vya mbegu na kuzuia nzi weupe kufika kwenye mimea.
  • Fanya mazoea ya kubadilisha mazao na mimea isiyoshambuliwa.
  • Epuka kupanda mimea mbadala karibu na mazao.
  • Weka matandazo kwenye kitalu cha mbegu au shamba ili kuvunja mzunguko wa maisha ya nzi mweupe.
  • Tumia mitego ya plastiki yenye kunata ili kunasa wadudu kwa wingi.
  • Fuatilia shamba, chagua mimea yenye magonjwa kwa mikono na uizike mbali na shamba.
  • Tafuta na tokomeza magugu ndani na nje ya shamba.
  • Lima kwa kufukia kwa kina uchafu wote wa mimea baada ya kuvuna au uchome moto.

Pakua Plantix