TSWV
Kirusi
Dalili ya awali ni kubabuka kwa majani machanga na madoa ya zambarau au kahawia kwenye majani. Kawaida inaonekana kwenye sehemu ya juu ya mmea. Michirizi ya zambarau na madoa madogo ya rangi ya kahawia huonekana kwenye shina na majani machanga, wakati mwingine hutengeneza miduara yenye kitovu cha pamoja. Kadili yanavyo ungana, huunda kiraka kikubwa kwenye ubapa wa jani, hatimaye kufa kwa tishu. Michirizi ya kahawia iliyokolea inaweza kuonekana kwenye shina na vikonyo. Ncha zinazo kua kwa kawaida huathiriwa sana na kufa kwa tishu za kimfumo. Mimea huonyesha ukuaji uliodumaa au inaweza kuonyesha ukuaji wa upande mmoja. Mimea iliyo athiriwa zaidi huzaa matunda ambayo hayakomai yenye miduara ya kijani hafifu yenye madoadoa na sehemu zilizoinuliwa. Juu ya matunda yaliyoiva, mekundu, miduara ya kahawia inayovutia ikiambatana na madoa ya njano na madoa hufanya matunda yakose soko.
Baadhi ya wadudu wanaowinda wadudu wengine hula lava au pupa wa vithiripi na wanapatikana kibiashara. Kwa aina zinazoshambulia majani na sio maua, jaribu mafuta ya mwarobaini au spinosad, haswa kwenye sehemu za chini za majani. Matumizi ya Spinosad ni mazuri sana lakini inaweza kuwa na sumu kwa maadui fulani asilia (k.m., Utitiri wawindaji, Lava wa nzi syrphid, nyuki) na yanapaswa kuepukwa wakati wa maua. Katika kesi ya mashambulizi ya vithiripi wa maua, baadhi ya utitiri wawindaji au lava wa kijani wa mbawakimia wanaweza kutumika. Mchanganyiko wa viziduo vya kitunguu saumu na baadhi ya dawa za kuua wadudu pia zinaonekana kufanya kazi vizuri.
Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kutokana na viwango vya juu vya uzazi na mzunguko wa maisha yao, vithiripi wamejenga ukinzani dhidi ya makundi mbalimbali ya dawa. Dawa za wadudu zinazofaa ni pamoja na azadirachtin au pyrethroids, ambazo katika bidhaa nyingi huunganishwa na piperonyl butoxide ili kuongeza ufanisi wake.
Virusi vya mnyauko wa madoadoa vya nyanya(TSWV) huenezwa na aina mbalimbali za vithiripi, ikiwa ni pamoja na vithiripi wa maua ya magharibi (Frankliniella occidentalis), vithiripi wa vitunguu (Thrips tabaci) na vithiripi wa pilipili (Scirtothrips dorsalis). TSWV pia amilifu katika wadudu wasambazaji kama vithiripi na inaweza kuisambaza kwa mfululizo. Tunutu wanaopata virusi kwa kula mimea iliyoambukizwa watabaki na uwezo wa kusambaza virusi kwa maisha yao yote. Hata hivyo, TSWV haiwezi kupitishwa kutoka kwa majike walioambukizwa hadi kwenye mayai. Virusi vina aina nyingi za mimea mwenyeji, ikiwa ni pamoja na nyanya, pilipili, viazi, tumbaku, lettuce na mimea mingine mingi.