ULCV
Kirusi
Jani la tatu la miche linalotokana na mbegu zilizoambukizwa huwa kubwa zaidi kuliko ilivyo kawaida. Majani haya yana rangi ya kijani hafifu kuliko kawaida. Vikonyo vinaweza kuwa vifupi na mishipa ya majani kuwa minene, yenye mabadiliko ya rangi kuwa nyekundu. Mwezi mmoja baada ya kupanda, majani huanza kusinyaa na kukunjamana, na kuwa na sura yenye mkwaruzo mithili ya ngozi. Mimea iliyoambukizwa kwa njia ya wadudu wanaosambaza magonjwa katika hatua za mwisho za ukuaji, kwa kawaida huonyesha dalili kwenye majani machanga, wakati majani yaliyokomaa yanakuwa hayana dalili. Majani huonesha ubadilikaji dhahiri wa rangi ya mishipa na kuwa ya njano, na maua yanaharibika umbo. Vitumba vya maua huwa vidogo na mmea hudumaa. Katika maua machache yanayozalisha, mbegu zilizobadilika rangi na zilizoongezeka ukubwa zinaonekana. Rutuba ya chavua na utengenezwaji wa maganda huathirika kwa kiasi kikubwa, na kusababisha upoteaji mkubwa wa mavuno.
Mbinu mbalimbali za kibiolojia zinaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Matumizi ya Dawa ya Pseudomonas fluorescens ambayo hutumika kwa kupulizia kwenye udongo au majani inaweza kusaidia kudhibiti idadi ya wadudu wasambazaji wa vimelea. Imeonekana kwamba siagi mbichi ya maziwa na kasini (protini kuu ya maziwa) vina athari katika usambazaji wa ugonjwa. Dondoo za mimea kama Mirabilis jalapa (ua la saa kumi), Catharanthus roseus (kwa jina lingine macho angavu au mmea wa makaburini), Datura metel, Bougainvillea spectabilis, Boerhaavia diffusa, na Azadirachta indica, zimekuwa na athari kwenye matukio ya maambukizi ya virusi shambani.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua zenye kinga pamoja na tiba za kibaiolojia endapo zinapatikana. Hakuna tiba ya kemikali dhidi ya virusi inayopatikana kwa sasa, lakini dawa za kuua wadudu (ambazo hufyonzwa na mmea na kutengeneza sumu dhidi ya wadudu) zinaweza kutumika kudhibiti idadi ya wadudu wanaosambaza vimelea. Inapendekezwa matumizi ya dawa za kuua wadudu zinazotokana na imidacloprid 70 WS @ 5 ml/kg. Dawa za kuua wadudu zinazotokana na dimethoate ambazo hutumika kwa kupulizia kwenye majani nazo pia zinaweza kutumika. Mchanganyiko wa 2,4-dixohexahydro 1,3,5-triazine (DHT) huzuia usambazaji wa virusi na huongeza muda wa kuatamiza kwa virusi.
Virusi hivi mara nyingi husambazwa na mbegu, na hivyo kusababisha maambukizi ya awali kwenye miche. Maambukizi ya upili kutoka mmea mmoja hadi mwingine hutokea kupitia wadudu wanaosambaza vimelea ambao hufyonza utomvu wa mmea, kama vile baadhi ya spishi za vidukari(mfano, Aphis craccivora and A. gossypii), nzi mweupe(Bemisia tabacci), na mbawakawa mla-majani(Henosepilachna dodecastigma). Kiwango cha usambaaji wa virusi na ukali wa ugonjwa hutegemea na kiwango cha uvumilivu wa mimea dhidi ya virusi husika, uwepo wa wadudu wasambazaji wa virusi shambani na hali ya hewa iliyopo. Virusi vinaweza kupunguza mavuno kutoka asilimia 35 hadi 81, kutegemea na wakati wa maambukizi.