Muwa

Batobato ya Miwa

SCMV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Muundo wa nakshi yenye mpangilio kwenye bapa za majani machanga.
  • Michirizi myembamba iliyobadilika rangi inayoambaa sambamba na mishipa ya jani.
  • Kufa kwa tishu kwenye majani ya zamani.
  • Sehemu zenye rangi nyekundu kwenye majani ya zamani.
  • Ukuaji uliodumaa na mashina tasa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Muwa

Dalili

Mimea michanga huonyesha dalili za wazi zaidi. Mimea iliyoambukizwa hutengeneza muundo wa kipekee wa nakshi wenye rangi ya kijani hafifu hadi mabaka ya njano yaliyopachikwa kwenye rangi ya kijani kibichi. Wakati mwingine kuonekana kwa muundo wa nakshi kunaimarishwa na michirizi myembamba iliyobadilika rangi inayoambaa sambamba na mishipa ya jani. Katika baadhi ya matukio, mistari pia inaweza kuonekana katika mashina machanga. Baadaye, majani yanaonyesha kubadilika rangi kwa ujumla, na michirizi inakuwa mikubwa na mingi zaidi. Mimea inapokaribia kukomaa, uwekundu kwa sehemu au kufa kwa tishu hutokea kwenye ubapa wa jani. Kulingana na wakati wa maambukizi, mimea inaweza kudumaa sana au kuwa tasa kabisa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dhibiti mimea yenye uwezekano wa kuhifadhi virusi kama vile magugu, shambani na maeneo jirani. Fuatilia na udhibiti idadi ya vidukari wanaweza kuambukiza mimea yenye afya na virusi hivi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Usitumie dawa za kuua wadudu ili kudhibiti idadi ya vidukari kwa sababu hii imeonekana kuwa haifanyi kazi.

Ni nini kilisababisha?

Vidukari husambaza virusi kupitia ulaji na vinaweza kuambukiza mimea yenye afya kwa siku kadhaa. Usambazaji kwa mitambo kutoka mmea hadi mmea pia unawezekana, virusi vinaweza kuletwa kwenye majani kupitia majeraha. Usambazaji wa mitambo kupitia visu au zana zingine hauwezekani kwa sababu kirusi haishi kwa muda mrefu nje ya tishu za mmea.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina sugu.
  • Panda mbegu zisizo na magonjwa kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Hakikisha idadi nzuri ya wadudu wenye manufaa ambao hula vidukari.
  • Fuatilia idadi ya mimea iliyoambukizwa.
  • Zuia uharibifu na majeraha kwenye mimea.

Pakua Plantix