PPSMV
Kirusi
Katika hatua ya awali ya ugonjwa huo, mishipa ya majani machanga hugeuka kijani nyepesi/iliyopauka. Katika maendeleo zaidi muundo wa nakshi za kijani iliyopauka na kijani kibichi hutokea. Majani na matawi huwa madogo, ambayo huupa mmea mwonekano uliodumaa na kuwa kama kichaka. Mimea inaweza isitoe maua au maganda/matunda.
Matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi hayawezekani, lakini inawezekana kupunguza hatari ya kuambukizwa kupitia utitiri. Wadudu wawindaji wa utitiri hupatikana mara kwa mara katika mazingira sawa na aina ya Brevipalpus. Michanganyiko iliyo na fangasi wa entomopathojeni wa jenasi ya Metarhizium au Hirsutella thompsonii pia inaweza kutumika kupunguza idadi ya utitiri.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi hayawezekani, lakini inawezekana kupunguza hatari ya kuambukizwa kupitia utitiri. Unaweza kupaka dawa za utitiri kama vile Kelthane, Tedion @1 ml kwa lita moja ya maji ili kuua utitiri.
Dalili husababishwa na Virusi Nakshi vya Utasa. Virusi huambukizwa kupitia utitiri wa Eriophyid. Hatari ya maambukizi huongezeka wakati mbaazi zinapopandwa mseto na ulezi au mtama. Katika vipindi vya joto na ukame, dalili hukomeshwa, wakati kivuli na unyevu huchochea kuongezeka kwa virusi.