MSV
Kirusi
Dalili hutofautiana kidogo kutegemea na aina ya mbegu za mmea na hali ya mazingira. Katika hatua za awali za maambukizi, madoa madogo ya duara yenye rangi ya manjano yanaweza kupatikana kwenye kitako cha majani machanga. Kadri ugonjwa unavyoendelea, idadi ya madoa huongezeka na huwa na tabia ya kuungana. Kwa aina za mimea inayoathirika kwa urahisi zaidi kuhimili ugonjwa, madoa hayo hugeuka kuwa mistari myembamba, meupe hadi ya manjano ambayo hukua sambamba na mishipa ya majani. Ikiwa maambukizi yatatokea mapema wakati wa ukuaji wa mmea, mistari hiyo hufunika jani lote na kusababisha mmea kudumaa, ukuaji usiokamilika wa maua na mahindi, pamoja na upungufu wa kujaza nafaka.
Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya Virusi vya Michirizi Kwenye Majani ya Mahindi(yaani Maize Leaf Streak Virus) kwa sasa. Tafadhali wasiliana nasi endapo utapata taarifa kuhusu njia yoyote inayoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.
Daima zingatia mbinu jumuishi zinazohusisha na kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali kwa magonjwa yanayosababishwa na virusi. Kupunguza idadi ya wadudu wanaoeneza virusi kwa kawaida husaidia kupungua kwa kiwango cha maambukizi. Bidhaa za madawa zinazotokana na dimethoate zinaweza kutumiwa kwenye majani, lakini njia hii inapaswa kutathminiwa kwa uangalifu dhidi ya hasara inayoweza kutokea kwenye mavuno, pamoja na hofu ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa.
Ugonjwa wa michirizi kwenye majani ya mahindi ni tatizo linalopatikana zaidi barani Afrika, lakini pia limeripotiwa kutokea kusini-mashariki mwa Asia. Uginjwa huu husababishwa na virusi vinavyoenezwa na baadhi ya spishi za viruka-jani (jamii ya panzi wadogo) waitwao kitaalamu Cicadulina. Wadudu hawa hupata virusi kwa kunyonya majani machanga yanayokua. Mzunguko wa maisha wa maisha yao huchukua kati ya siku 22 hadi 45, kutegemea na hali ya hewa. Joto la takriban 20-35°C ndilo muafaka kwa ukuaji wao, na hivyo kuongeza hatari ya maambukizi kwa mazao. Kundi kubwa la mazao ya nafaka hutumika kama mimea mbadala inayoweza kuhifadhi virusi, na mazao hayo ni kama ngano, shayiri, shairi, mtama.