Bunchy Top Virus
Kirusi
Virusi vinaweza kuathiri sehemu zote za mmea katika hatua zote za ukuaji. Dalili za awali zinaweza kudhaniwa kuwa upungufu wa virutubisho au mfadhaiko wa mmea. Dalili hizi ni pamoja na kuonekana kwa michirizi ya kijani iliyokolea kwenye vikonyo vya majani, mshipa wa kati wa majani pamoja na mishipa mingine ya jani. Aidha, michirizi hii huonekana upande wa chini ya majani mapya. Baadaye, eneo bapa la majani linaweza pia kuonyesha vijidoa vidogo vya kijani kibichi na michirizi kwenye mishipa (inayoitwa muundo wa msimbo wa Morse). Majani yaliyoathiriwa huonekana kudumaa, membamba na yaliyosimama, na yana ukingo wa uliojipinda na kuwa na tishu zilizokufa. Katika maambukizi ya juu, majani mapya yanaonyesha dalili hizo kuwa mbaya zaidi. Taji la mgomba huwa na mkusanyiko wa majani madogo ya kijani mpauko au manjano ambayo huunda shada la majani kwa juu. Ukuaji wa jumla unadumaa na mmea unaweza usitoe mkungu wa ndizi au matunda. Ikitokea matunda yanazalishwa, matunda hayo huharibika umbo na kuwa madogo.
Endapo ugonjwa utagundulika katika hatua za awali, kunyunyizia mimea kwa ukamilifu kwa kutumia maji ya sabuni au sabuni ya kuua wadudu kunaweza kusaidia kupunguza idadi ya vidukari. Dhibiti matumizi ya kemikali ili kudumisha uwepo wa maadui wa asili wa vidukari.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kikemikali ya moja kwa moja kwa magonjwa ya virusi. Idadi ya vidukari inaweza kudhibitiwa hadi kiwango fulani kwa kutumia cypermethrin, acetamid, chlorpyrifos au viua wadudu vinavyohusiana na hivyo. Kwa suala la kutambua na kuiondoa/kung'oa mimea yenye sifa tofauti na mingine, itibu kwa mafuta ya taa yenye nguvu au dawa ya kuua wadudu ili kuua vidukari wote.
Dalili hizo husababishwa na virusi vinavyoenezwa kutoka mti hadi mti au kati ya shamba na shamba ambapo virusi hao huenezwa na vidukari wa mgomba (Pentalonia nigronervosa). Uambukizaji kwenye umbali mkubwa unaweza kutokea kupitia ubebaji wa mimea iliyoambukizwa kutoka shamba moja hadi jingine. Mimea ambayo ni makazi ya virusi hawa ni pamoja na Tangawizi, Heliconia na Myugwa (Magimbi). Aina za migomba hutofautiana katika urahisi wake wa kuambukizwa, tofauti hiyo huonyeshwa hasa katika muda unaochukua kwa dalili kuonekana. Mimea haiponi kutokana na maambukizi. Maambukizi ya msingi kupitia miche iliyoambukizwa kwa ujumla ndio maambukizi mabaya zaidi kuliko maambukizi ya pili kupitia vidukari. Dalili pia huongezeka wakati wa majira ya kuchipua au wakati wa hali ya hewa ya joto na kavu.