BBrMV
Kirusi
Dalili iliyo wazi zaidi huonekana kwenye madunda ya shazi la maua likiwa kwenye muundo/mpangilio wa mozaiki nyekundu-kahawia. Madunda ni jina la majani madogo ambayo hufunika safu za maua kwenye kikonyo cha maua. Katika mimea michanga, vidonda nyenye umbo la msokoto (mithili ya mkono wa kisokotea nyuzi) vikiwa na rangi ya manjano au nyekundu-kahawia na michirizi vinaweza kupatikana kwenye vikonyo au mishipa ya katikati ya majani. Mara chache pia huonekana kwenye ubapa wa majani ikienda sambamba na mishipa au kwenye shina la vishada vya matunda. Wakati majani yaliyokufa yanapovutwa, mabaka ya rangi kahawia nyeusi au michirizi huonekana kwenye tishu za ndani. Kasoro za ukuaji kwenye mashada na matunda yaliyoharibika pia ni tabia ya ugonjwa huo. Virusi vinaweza kuenea haraka na maambukizi makali yanaweza kusababisha hasara katika mavuno na ubora wa matunda.
Dawa ya kudhibiti kuvu iitwayo verticillium lecanii inaweza kutumika kupunguza idadi ya vidukari. Sabuni ya kuua wadudu pia inaweza kutumika kudhibiti vidukari wakati idadi yao si kubwa sana.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi. Hata hivyo, matumizi ya dawa za kuua wadudu yanaweza kudhibiti idadi ya vidukari hadi kiwango fulani (kwa mfano cypermethrin, acetamid, chlorpyrifos). Dawa za kuulia wadudu zinaweza kutumika kuua mimea iliyoathiriwa au chipukizi machanga yanayokua kutoka kwa miti iliyokatwa.
Dalili husababishwa na virusi vinavyoathiri migomba katika hatua tofauti za ukuaji. Virusi vinaambukizwa kwa njia isiyodumu kwa aina kadhaa za spishi (aina) za vidukari. Virusi, vilivyopatikana kutokana na kula kwenye mimea iliyoambukizwa, huishi kwa muda mfupi tu kwenye vimelea vya magonjwa. Uhamisho au usafirishaji wa mimea iliyoambukizwa kati ya shamba na shamba ni njia nyingine ya kueneza maambukizi. Jina lake la kawaida linatokana na dalili za sifa za mosai kwenye madunda ya maua.