Ndizi

Kirusi wa Mchirizi wa Migomba

Banana Streak Virus

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Michirizi ya manjano kutoka katikati ya mshipa jani hadi kwenye ukingo.
  • Baadaye, rangi hii ya manjano hugeuka na kuwa kahawia au nyeusi, iliyoingiliwa au kukatizwa na madoa makubwa ya njano.
  • Kufa kwa kingo za majani kuelekea katikati ya mshipa.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Ndizi

Dalili

Dalili za ugonjwa huu zinaweza kutofautiana sana, kutegemea na aina na kiasi cha virusi vinavyohusika, aina ya mimea na hali ya kimazingira. Dalili ya kawaida ni kutokea kwa michirizi ya manjano iliyo kamili au iliyokatika ambayo hutokea katikati ya mshipa wa jani hadi kwenye ukingo. Michirizi hii baadaye hubadilika na kuwa ya kahawia au myeusi na inaweza kukatizwa na madoa makubwa ya manjano au yenye mpangilio wa umbo la macho. Ufaji wa tishu huanza kuonekana kwenye jani, kuanzia kwenye kingo, na wakati mwingine kuathiri mshipa wa kati wa jani na petiole(yaani kikonyo cha jani). Wakati mwingine, tishu za ndani za shina pia huathiriwa kwa kuoza. Dalili iliyotaja hapo juu inaonekana katika mazingira ya joto la chini na mchana mfupi. Sio tu majani yanayo athiriwa lakini pia ukuaji wa mmea kwa kawaida hudumaa, wakati ukubwa wa mkungu na matunda hupungua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu wanaodhibiti ueneaji wa vidung'ata; yaani kama vile nyigu kidusia, mbawakimia, au nzi waeleaji na wadudu-kibibi wanaweza kutumika kudhibiti idadi ya vidung'ata. Mafuta mepesi ya madini au mwarobaini vikinyunyiziwa kwenye majani pia zinafaa wakati vidung'ata ni wadogo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kikemikali ya magonjwa ya virusi. Nta ya ulinzi inayowafunika vidung'ata (vidukari-sufu) hufanya kuwa vigumu kuwaua. Matibabu kwa kutumia madawa ya kuua wadudu kama vile deltamethrin yanaweza kutumika kudhibiti idadi ya vidung'ata.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu unasababishwa na virusi. Asili ya dalili inabainika kwa mkusanyiko wa chembe chembe za virusi kwenye mimea. Hali ya joto, na hali ya hewa kwa ujumla, pia huvutia matokeo ya maambukizi. Virusi huenezwa kutoka mti hadi mti au kati ya shamba hadi kupitia aina kadhaa za vidung'ata (Pseudococcidae). Njia nyingine ya kueneza ugonjwa kwa umbali mrefu ni kwa kutumia nyenzo za kupandia zenye maambukizi au mbegu. Ugonjwa hauenezwi kwa njia ya udongo na hakuna uwezekano wa kusambazwa kupitia majeraha ya mimea yanayotokana na zana za kilimo wakati wa kazi za shambani. Ni tatizo la dunia nzima ambalo huathiri migomba na spishi zinazohusiana nayo, na ambalo linaweza kuathiri vibaya ukuaji wa mimea, mavuno ya matunda na ubora. Hamna uwezekano wa virusi kuenezwa kwenye zana za kukatia au kwa njia za mitambo.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia nyenzo za kupandia zisizo na virusi kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Mimea iliyoambukizwa inapaswa kukatwa na kuharibiwa.

Pakua Plantix