Papai

Batobato wa Papai

PapMV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Mfano wa picha mpangilio (nakshi) kwenye majani.
  • Majani yaliyoharibika kidogo umbile.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Papai

Dalili

Dalili za maambukizi hujilimbikiza kwenye majani machanga na ni pamoja na muundo wa nakshi kiasi wa jani na mabadiliko kidogo ya umbo. Madoa ya kijani kibichi kama vile malengelenge huonekana vinginevyo majani ya rangi ya manjano-kijani. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, mishipa ya majani inaweza kuonyesha dalili za kufutika/kupotea, vikonyo vya majani ni vifupi kwa kiasi fulani na majani hujikunja kuelekea chini huku yakiwa yamesimama wima. Sehemu zingine za mmea (shina, maua) haziathiriwa. Mimea huonyesha ukuaji uliodumaa kiasi, jambo ambalo hudhihirika tu linapolinganishwa moja kwa moja na mimea yenye afya.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Takasa zana za kazi au zipashe katika jiko 150 ° C kwa saa 1 ili kuua virusi. Zana za kufanyia kazi au glavu pia zinaweza kuzamishwa kwenye sodium hypochlorite 0.525% na kisha kusuuzwa kwenye maji.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na mbinu za kibayolojia ikiwa zinapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali kwa maambukizo ya virusi.

Ni nini kilisababisha?

Virusi hivyo huathiri mipapai pamoja na mazao mengine, kwa mfano, yale ya jamii ya maboga na matango (cucurbits). Huenea kutoka kwa mmea hadi mmea kupitia majeraha yanayosababishwa na matumizi ya zana za kilimo/mitambo. Njia nyingine ya ueneaji wa ugonjwa huu ni kupitia vipandikizi vilivyoambukizwa. Mara nyingi huambatana na magonjwa mengine ya virusi na dalili zinaweza kutofautiana kidogo katika matukio hayo. Virusi hivi kwa uhalisia vina madhara madogo katika papai lakini ikiwa hali zinazo wafaa zitakuwepo, wanaweza kusababisha hasara ya mavuno.


Hatua za Kuzuia

  • Panda mbegu au miche kutoka kwa mimea yenye afya au kutoka kwa vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Fanya mzunguko wa mazao kwa mzao yasiyo ya shambuliwa virusi hawa.
  • Jihadhari na kubeba udongo au mbegu/miche za mimea zilioambukizwa kwenda kwenye mashamba ambayo hayajaambukizwa.
  • Ainisha, ondoa na uharibu mimea iliyoambukizwa au sehemu za mimea.
  • Safisha/takasa zana na vifaa vyako kwa joto au njia zingine.
  • Hakikisha mikono na nguo ni safi na vaa glavu.

Pakua Plantix