Papai

Kirusi Mkunja Majani ya papai

PaLCV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Majani ya juu hujikunja kuelekea chini- na ndani.
  • Majani kuongezeka unene na kuficha mishipa.
  • Majani huwa kama ngozi na hukakamaa.
  • Upukutishaji majani husababisha ukuaji kudumaa.
  • Matunda machache, madogo yaliyo badilika umbo.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Papai

Dalili

Dalili za wazi zaidi za ugonjwa huu ni majani yaliyo jikunja kuelekea chini au ndani. Dalili zingine ni pamoja na unene wa mishipa ya majani, wakati mwingine kutokea kwa vinundu kwenye majani. Majani huwa kama ngozi na hukakamaa na vikonyo kubadilika umbo na kujisokota. Majani ya juu huathirika zaidi. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo upukutishaji wa majani unaweza kutokea. Ukuaji wa mmea hudumaa na uzalishaji wa maua au matunda unaweza kuathiriwa. Ikiwa ugonjwa upo kabisa, matunda ni madogo, yaliyoyo haribika umbile na huanguka mapema kabla hayaja komaa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyunyiza emulsion za mafuta meupe (1%) ili kuzuia vidukari kuchukua na kueneza virusi na.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali kwa maambukizi ya virusi. Hata hivyo, kudhibiti idadi ya inzi weupe kunaweza kupunguza ukali wa maambukizi. Uwekaji dawa kwenye udongo wakati wa kupanda na unyunyuziaji majani mara 4-5 kwa kutumia metasystox kwa muda wa siku 10 vinaweza kudhibiti kwa ufanisi idadi ya nzi weupe.

Ni nini kilisababisha?

Msambazaji kuu wa maambukizi ya virusi hawa ni nzi weupe waitwao Bemisia tabaci. wanaeneza virusi kutoka kwa mmea hadi mmea kwa njia isiyo na mwendelezo. Hii ina maana kwamba maambukizi hufanyika ndani ya sekunde chache wakati virusi bado wakiwa hai kwa msambazaji. Njia nyingine za kuenea kwa ugonjwa huu ni kupitia miche au mbegu zilizoambukizwa na vile vile kupitia vipandikizi. Virusi vya kujikunja kwa majani ya mpapai haviambukizwi kupitia matumizi ya mitambo shambani. Mimea mbadala inayohifadhi/kushambuliwa na virusi hawa ni nyanya na mimea ya tumbaku. Virusi hawa wamesambaa sana lakini hadi leo wana matukio machache. Hata hivyo, katika baadhi ya matukio maalum, wanaweza kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina sugu zinazopatikana.
  • Usikuze mimea mbadala inayohifadhi/kushambuliwa na kirusi huyu karibu na mipapai.
  • Epuka matumizi ya viua wadudu kupita kiasi ili kuvutia wadudu wenye faida.
  • Ng'oa mimea iliyoambukizwa na kuiharibu.
  • Kuwa mwangalifu usiache mabaki yoyote ya mimea baada ya kuvuna.

Pakua Plantix