PRSV
Kirusi
Dalili zinaweza kutofautiana kidogo kulingana na umri wa mmea wakati wa maambukizi, nguvu ya mmea na nguvu ya virusi. Miundo kama vile malengelenge ya kijani kibichi huonekana kwanza kwenye majani. Baadaye, miundo hiyo hukua katika muundo wa madoadoa katika vivuli tofauti vya kijani. Katika hatua za baadaye za ugonjwa, majani yana mwonekano wa kamba ya kiatu na huonyesha muundo wa nakshi na madoa ya manjano na kahawia yenye seli mufu. Ukubwa wa majani hupungua kwa kiasi kikubwa, hivyo kusababisha kudumaa kwa ukuaji na mwavuli/kivuli kidogo. Madoa ya njano yaliyo tota maji na michirizi ya mafuta pia huonekana kwenye shina na vikonyo. Matunda yaliyoambukizwa huonyesha madoa mengi ya kijani kibichi, ambayo mara nyingi yamezama, yenye mng`ao yenye saizi iliyopungua na umbo lililo haribika. Ikiwa maambukizi yatatokea katika hatua za awali, matunda hayawezi kuwa na soko.
Nyunyiza emalshani (emulsion) za mafuta meupe kwa viwango vya 1% ili kuzuia kubebwa na kuenezwa kwa virusi na vidukari. Mchanganyiko wa viumbe wadogo wenye manufaa ikiwa ni pamoja na baadhi ya aina ya bakteria, hamira, actinomycetes na bakteria photosynthetic unaweza kupunguza matukio ya ugonjwa huo.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali ya moja kwa moja kwa maambukizi ya virusi. Hata hivyo, dawa ya majani ya di-methoate au azadirachtin inaweza kupunguza idadi ya vidukari. Weka dawa kila baada ya wiki mbili baada ya dalili za kwanza kuonekana.
Virusi huenezwa na spishi nyingi za vidukari kwa njia isiyo na mwendelezo. Kwa kuwa virusi hawazaliani ndani ya vidukari, maambukizi kutoka kwa mmea hadi mmea lazima yatokee ndani ya muda mfupi (sio zaidi ya dakika moja). Virusi hivyo vina aina mbalimbali za mimea mbadala inayo wahifadhi kama vile tikiti maji na mimea mingine jamii ya maboga na matango, lakini shabaha yake kuu ni papai. Maambukizi yanaweza kuenea kwa haraka katika shamba ikiwa yataambatana na idadi kubwa ya vidukari wenye mabawa. Hali ya hewa ya baridi pia inaweza kuzidisha dalili kwenye majani (muundo wa nakshi na uharibifu wa umbo la majani).