MYMV
Kirusi
Majani machanga yanaweza kupoteza rangi ya kijani (klorosi), kujikunja kuelekea chini, au kuwa na rangi nyeupe kama karatasi. Majani ya zamani yanaonyesha madoa ya njano yaliyosambaa ambayo baadaye hugeuka kuwa mabaka ya rangi ya kijani na manjano yasiyo na umbo maalumu. Sehemu za kijani zinainuka kidogo, na kufanya jani kuwa na muonekano wa mikunjo. Vidonda huongezeka ukubwa na kuungana, kisha tishu huanza kufa (nekrosi). Ukuaji wa mimea iliyoathirika hudumaa. Mimea hii hutoa maua na maganda machache. Maganda yake ni madogo, membamba na yanakuwa na madoa, na wakati mwingine hujikunja kuelekea juu. Aidha, huwa na mbegu chache na ndogo.
Hakuna hatua za udhibiti wa kibaiolojia zinazoweza kuchukuliwa kudhibiti magonjwa yanayosababishwa na virusi. Hata hivyo, dondoo za mimea kama vile mafuta ya mwarobaini yana ufanisi katika kupunguza idadi ya nzi weupe na kuboresha mavuno ya mazao yaliyoathirika.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Kupulizia majani kwa cypermethrin, deltamethrin, au dimethoate inaweza kupunguza idadi ya nzi mweupe. Ili kupunguza wadudu wanaosambaza ugonjwa huu, mazao ya kutengeneza mipaka (mahindi, mtama na ulezi) yanaweza kutibiwa kwa dawa za kuua wadudu.
Virusi huenezwa na nzi mweupe anayefahamika kitaalamu kama Bemisia tabaci. Maambukizi ya mbegu hayawezekani. Ugonjwa huu unapatikana katika nchi kadhaa barani Asia na Australia. Mabaka ya njano kwenye majani hupunguza tija ya mimea kwa kiasi kikubwa. Joto la vuguvugu na unyevu mwingi husaidia kuongezeka kwa idadi ya wadudu wanaosambaza ugonjwa huu. Maambukizi ya batobato ya njano ya choroko yanaweza kusababisha upotevu wa mavuno wa hadi asilimia 100. Batobato ya njano ya choroko huathiri choroko nyeusi mara nyingi zaidi kuliko choroko za kijani.