GBNV
Kirusi
Dalili ya msingi ya ugonjwa huo ni madoa kidogo ya manjano kwenye vipande vya majani vichanga, ambayo baadaye hukua na kuwa madoa ya mduara wa manjano wenye tishu zilizo kufa na michirizi. Kufa kwa tishu baadaye huenea hadi kwenye vikonyo, na kuelekea juu ya shina hadi kwenye chipukizi la juu kwenye ncha ya mmea, na kusababisha kuoza kwa miundo ya maua, hivyo jina la ugonjwa wa muozo wa chipukizi la juu la karanga likatokea. Hali hii husaidiwa na halijoto ya juu ya wastani. Mimea iliyoambukizwa huonyesha ukuaji wa kudumaa, kugeuka kuwa na rangi ya njano kwa ujumla, kuenea kwenye mashina mapya na uharibifu wa majani mapya. Vigingi vinaweza kuwa na madoadoa na kubadilika rangi na kuwa na mbegu ndogo zilizonywea na madoa juu yake. Hasara za mavuno huonekana endapomimea imeambukizwa katika hatua za mwanzo.
Kunyunyizia viziduo vya mmea wa mtama au jani la mnazi siku 20 baada ya kupanda kuna ufanisi katika kudhibiti idadi ya vithiripi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia yanayopatikana. Matibabu ya kemikali ya maambukizi ya virusi hayawezekani. Hata hivyo, baadhi ya matibabu yanapatikana kwa udhibiti wa vithiripi wanaoeneza virusi. Kunyunyizia viua wadudu kama thiamethoxam siku 30-35 baada ya kupanda kama hatua ya kuzuia kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya muozo wa chipukizi la juu la karanga. Matibabu ya mbegu kwa imidacloprid @ 2ml/1kilo ya mbegu pia yanafaa dhidi ya vithiripi.
Ugonjwa wa muozo wa chipukizi la juu la karanga husababishwa na virusi. Uvamizi wa mimea ni endelevu na hutegemea aina ya wadudu (Thrips palmi) ambao hula tishu za mimea na utomvu. Kwa kukosekana kwa mimea ya karanga, vithiripi hula na kuvamia mimea mbadala ndani au karibu na shamba, kwa mfano marigold ya kusini (Tagetes minuta), na klova ya chini ya ardhi (Trifoleum subterraneum). Kwa hivyo, kuondolewa kwa mimea hii ni muhimu sana kudhibiti idadi ya wadudu. Kupanda karibu karibui pia huzuia vithiripi kutua kwenye zao la karanga.