PVY
Kirusi
Dalili za maambukizi hutofautiana kulingana na aina, umri wa mimea na hali za kimazingira. Miundo ya nakshi ya manjano hadi ya kijani kibichi huonekana kwenye ubapa wa majani, na kuyapa mwonekano wenye madoadoa na ulioharibiwa, mara nyingi kuanzia kwenye ncha. Mistari ya kahawia hadi mweusi na madoa ya mviringo ya tishu zilizokufa hujitokeza kwenye mishipa ya majani na mashina machanga. Machipukizi na maua hayakui zaidi. Viazi kutoka kwenye mimea iliyoambukizwa ni vidogo na vinaweza kuwa na miduara yenye tishu zilizokufa kwenye ngozi. Ukuaji wa mmea wote hutatizwa na mavuno ya mazao yanapungua.
Matumizi ya kila wiki ya mafuta ya madini yanaweza kupunguza kuenea kwa virusi. Yanapunguza kasi ya kuambukizwa kwa virusi na vidukari na kurekebisha tabia yao ya kula, na kuwafanya wasiwe na uwezekano wa kuambukiza mimea.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali ya magonjwa ya virusi hayawezekani. Hata hivyo, dawa za kuua wadudu zinaweza kutumika kupunguza idadi ya vidukari
Kirusi huyu haambukizi sana. Huathiri zaidi mimea ya familia ya solanaceous, kama vile nyanya, viazi na pilipili. Anaezwa kupitia aina mbalimbali za vidukari wenye mabawa, mimea iliyoathiriwa na zana zilizoambukizwa.