PLRV
Kirusi
Dalili zinazoonekana hutofautiana kulingana na aina ya mimea, hali ya mazingira na aina ya maambukizi. Maambukizi ya msingi, ambayo husababishwa na vidukari, huonekana zaidi kwenye majani machanga. Kingo za jani huanza kujiviriga kuelekea juu na kuwa kavu, kupauka au kubadilika rangi na kuwa njano katikati ya vishipa jani. Kwenye mimea iliyo oteshwa kutokana na kiazi chenye vimelea (maambukizi ya upili), majani ya zamani yamejikunja kuelekea juu, magumu na yaliyokakamaa yenye rangi ya zambarau au nyekundu upande wa chini, huku majani machanga yakiwa yamesimama wima yenye rangi ya kijani kilicho fifia au manjano. Ukuaji wa mimea uliodumaa na mabua ni magumu na yaliyo simama wima. Viwango vya juu vya maambukizi hupunguza mavuno ya viazi na soko.
Matibabu ya moja kwa moja ya virusi hayawezekani, lakini kupunguza idadi ya vidukari kwa njia ya wadudu wanaokula wadudu wengine au wadudu vimelea(wanyonyaji) ni hatua ya kuzuia yenye manufaa. Wadudu kobe, mende askari, mbawakimia, na baadhi ya aina ya mbu usubi na nzi hula vidukari wakubwa na lava. Nyigu wanyonyaji pia wanaweza kutumika.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali ya magonjwa ya virusi hayawezekani. Walakini, idadi ya vidukari inaweza kudhibitiwa kwa kiwango fulani. Weka viua wadudu katika awamu za mwanzo za ukuaji wa mazao kama mfano.
Ueneaji wa awali hutokea wakati mimea inaposhambuliwa na kuliwa na vidukari vinavyobeba virusi wakati wa msimu wa ukuaji. Maambukizi ya upili hutokea endapo viazi vilivyopandwa vilikua na vimelea, na mimea ya viazi ikaota kutoka kwenye mbegu hizo. Vidukari husambaza maambukizi kwa mimea mingine yenye afya. Virusi hudumu kwenye maisha ya vidukari, hivyo uwezekano wa kuambukiza ni mkubwa. Ili kusambaza virusi, vidukari wanahitaji kula kwenye mmea kwa angalau masaa 2. Udongo wenye unyevunyevu huongeza hatari ya kuambukizwa.