CGMMV
Kirusi
Katika hatua za awali za ugonjwa, madoa ya kijani iliyofifia au ya njano na kupotea kwa rangi ya kijani kwenye mishipa ni dalili zinazoweza kuonekana kwenye majani machanga. Maambukizi makali husababisha kutokea kwa madoa ya njano, kujikunja na kuharibika umbo la majani pamoja na mmea kudumaa na katika hatua za baadae za ukuaji, tishu za majani hufa. Majani yaliyokomaa yanaweza kupauka rangi au kuwa na rangi ya njano yenye weupe na kudondoka kabla ya wakati. Dalili kwenye matunda zinatofautiana kuanzia katika kutoonesha kabisa kwa dalili (angalau kwa nje) hadi kuwa na madoa au michirizi mikali, kupotoka kwa umbo, au kudondoka. Dalili za baadae zinaonekana zaidi katika hali ya joto la juu. Katika mazingira fulani fulani, tunda lisiloonesha dalili za nje, kwa ndani linaweza kuwa na mabadiliko ya rangi ndani au kuwa na tishu zilizokufa. Matunda kuanguka kabla ya wakati pia ni kawaida.
Ikiwa utatibu mbegu kwa joto kavu la 70°C kwa hadi muda wa siku tatu, mbegu hizo hazitakuwa na chembe hai za virusi, lakini bado zitakuwa na uwezo wa kuota. Tumia vifaa vya majaribio ya batobato wa matango, endapo vinapatikana. Tumia dawa za kuua wadudu za kikaboni zinazolenga wadudu wanaotafuna.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Matumizi ya dawa za kuua wadudu ambazo zinalenga wadudu wanaotafuna zinaweza kuzuia kuenea kwa virusi. Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya magonjwa ya virusi kama virusi vya batobato wa matango.
Dalili husababishwa na virusi vya batobato ya matango (CGMMV), virusi ambavyo huathiri mazao jamii ya maboga, ikiwemo tango, tikiti maji, na tikiti tamu. Virusi hivi vinaweza kubaki hai kwa muda mrefu sana kwenye mabaki ya mimea iliyokufa kwenye udongo. Uambukizaji hutokea kupitia mbegu zilizoathirika, majeraha kwenye mimea yaliyosababishwa na zana za kukata, zana za kilimo, na kupitia wadudu wanaotafuna kama vile mbawakawa/mbawakavu. Virusi hivi pia vinaweza kusambazwa kutoka mmea mmoja hadi mwingine kupitia vipandikiz au kazi nyingine za shamba zinazoweza kujeruhi mmea. Wadudu wanaofyonza (mfano, vidukari, utitiri, na nzi weupe) hawasambazi virusi hivi. Mara mmea unapopata maambukizi, hakuna tiba inayojulikana dhidi ya virusi hivi. Hususani kwenye vitalu nyumba, idadi ya maambukizi kutokana na virusi hivi inazidi kuongezeka.