CMV
Kirusi
Dalili hutofautiana kutegemea na aina ya mmea iliyoathirika na hali ya mazingira. Katika hali fulani, virusi vinaweza kuwepo lakini dalili zake zisionekane. Mabaka ya manjano au madoa ya kijani hafifu na manjano yanaweza kuonekana kwenye majani na matunda. Ukuaji wa wima wa matawi ya pembeni na vikonyo vya majani huongezeka, na kusababisha majani na vikonyo kupinda kuelekea chini. Majani machanga yanaonekana kujipinda na kuwa membamba, na mmea mzima hudumaa na kuchukua umbo lisilo la kawaida, na kuwa na mwonekano mithili ya kichaka. Maua yanaweza kuonyesha mistari myeupe. Matunda hutengeneza uvimbe juu, unaoyafanya yasiuzike.
Matumizi ya dawa za kupulizia za mafuta ya madini kwenye majani yanaweza kuzuia vidukari kula majani hayo na hivyo kudhibiti idadi yao.
Daima zingatia mbinu jumuishi zeneye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Hakuna dawa za kikemikali zenye ufanisi dhidi ya batobato, wala hakuna zinazoweza kukinga mimea dhidi ya maambukizi. Dawa za kuua wadudu zenye cypermethrin au chlorpyrifos zinaweza kutumika kama dawa ya kupulizia majani dhidi ya vidukari.
Dalili zinazosababishwa na batobato wa tango, ambavyo vinaathiri aina mbalimbali za mimea (mazao ya jamii ya maboga, mchicha, mboga ya saladi, pilipili na figili pamoja na aina nyingi za maua, hasa myungiyungi, delphiniums, primulas na daphnes). Virusi hivi vinaweza kubebwa na kuenezwa na aina tofauti 60-80 za vidukari. Njia nyingine za kueneza ni pamoja na mbegu na vipandikizi vilivyoathirika, na uhamishaji kupitia mikono ya wafanyakazi au zana za kazi. Batobato wa tango inaweza kuishi msimu wote wa baridi kwenye magugu ya maua yanayodumu zaidi ya mwaka, na mara nyingi pia kwenye mazao yenyewe, katika mizizi, mbegu au maua. Katika maambukizi ya awali, virusi vinakua sehemu yote ya ndani ya miche mipya inayojitokeza na kufika hadi kwenye majani ya juu. Vidukari wanaokula mimea hii hubeba na kueneza virusi hivyo hadi kwenye mimea inayohifadhi virusi vya batobato (maambukizi ya pili). Virusi vinatumia tishu za mishipa ya mmea inayovihifadhi kwa kusafiri umbali mrefu kati ya viungo tofauti vya mimea.