Maharage

Virusi vya Batobato ya Kunde

BCMV

Kirusi

Kwa Ufupi

  • Muundo wa nakshi yenye rangi za kijani iliyofifia na kijani kibichi kwenye majani.
  • Majani yaliyo simama wima, yaliyojikunja au yaliyobadilika umbo.
  • Majani kujikunja kuelekea chini.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Maharage

Dalili

Awali, vipande vitatu vya jani la mharage huwa na rangi iliyofifia kidogo. Taratibu, muundo wa nakshi yenye rangi za kijani iliyofifia na kijani kibichi hutokea kwenye uso wa majani (nakshi ya kijani juu ya kijani). Baadhi ya mishipa ya majani au sehemu yake huonyesha dalili za kubadilika rangi na kuwa ya manjano. Kadri ugonjwa unavyoendelea, sehemu za majani zinaweza kukunjamana, kuwa na malengelenge au kubadilika umbo. Majani yanayojikunja kuelekea chini au kuvirigwa ni dalili nyingine za baadae. Mimea iliyoathirika katika hatua za awali za ukuaji inaweza kudumaa kwa kiasi kikubwa na kutozaa, ikiwa na maganda/vitumba vichache na mbegu chache kwa kila kitumba. Kwa baadhi ya aina za mbegu zinazoweza kuathiriwa, virusi vinaweza kusababisha kuoza kwa mizizi, dalili ambayo huonekana tu katika joto la zaidi ya 30°C.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya moja kwa moja ya virusi hayawezekani. Mafuta ya madini yaliyozimuliwa yanaweza kupunguza usambazaji wa virusi na vidukari, lakini mafuta haya yakiwa katika hali ya kukolea sana (yaani yasiyozimuliwa) , yanaweza kuwa sumu kwa mimea.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia yanayowezekana. Matibabu kwa kutumia madawa ya kemikali kwa maambukizi ya virusi hayawezekani. Udhibiti wa vidukari wanao eneza virusi kwa kutumia madawa ya kemikali mara nyingi hakufanyi kazi vizuri.

Ni nini kilisababisha?

Chanzo kikuu cha maambukizi ni mbegu zilizoathirika. Mambukizi ya upili kutoka kwenye mmea mmoja hadi mwingine hutokea kupitia chavua iliyoathirika, wadudu wahamishao magonjwa (hususani vidukari) au kupitia majeraha ya mmea yanayosababishwa na zana za kilimo wakati wa kazi shambani. Dalili na athari kwenye mavuno hutegemea aina ya mmea, hali ya mazingira (joto na unyevunyevu) na muda wa maambukizi. Maharage yatambaayo chini (runner beans) yameonekana kutodhurika na virusi, wakati maharage yanayotambaa kwenye miti/fito ndefu (pole beans) na maharagwe ya kawaida (bush beans) yapo kwenye hatari zaidi ya kuathirika. Hasara ya hadi 100% inaweza kutokea kwenye mimea inayo ambukizwa kirahisi inayokuzwa kutoka kwenye mbegu zenye virusi (maambukizi yanayosababishwa na mbegu). Maambukizi ya baadaye kwa vidukari kwa kawaida ni hafifu zaidi. Katika joto la zaidi ya 30°C, dalili huwa mbaya zaidi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya kutoka vyanzo vilivyothibitishwa.
  • Panda aina za mbegu zinazostahimili ugonjwa kadri inavyowezekana.
  • Panda karibu karibu ili kuzuia vidukari kuingia kwenye mwamvuli wa majani.
  • Panda mapema ili kuepuka idadi kubwa ya vidukari.
  • Ondoa mimea iliyoathirika pale dalili za kwanza zinapoonekana.
  • Lima maharage mbali na maeneo mengine ya uzalishaji wa mazao jamii ya maharage.
  • Fanya mzunguko wa mazao kwa mimea isiyohifadhi magonjwa.
  • Panda mazao rafiki ili kuzuia vidukari.

Pakua Plantix