Komamanga

Upele wa Komamanga

Elsinoë punicae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Kutokea kwa mabaka makavu na yenye ukakasi kwenye maua na matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Komamanga

Dalili

Dalili huonekana kama madoa yenye kutu kwenye matunda ambayo baadaye huwa na vidonda vya kigaga/upele. Madoa hupanuka na kuungana na kutengeneza dalili kama kigaga/upele na kizibo huonekana kwenye maua na matunda (machanga na yaliyokomaa). Ugonjwa huo unaweza kusababisha kuharibika kwa umbo la matunda machanga pamoja na kuvuruga uchavushaji. Rangi ya kipele ni kijivu au kahawia. Hakuna dalili za ugonjwa ndani ya matunda zinazoonekana. Vidonda vya kahawia kwenye majani na matawi vinaweza kuonekana lakini sio tabia ya ugonjwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo hakuna udhibiti wa kibiolojia unaofaa na unaotumika ambao umeripotiwa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ingawa kuna madai ya ukosefu wa taarifa juu ya usimamizi wa kemikali, baadhi ya dawa za kunyunyuzia vimelea zinaonekana kuwa na matokeo mazuri. Hasa carbendazim (0.1%), thiophanate methyl (0.1%), bitertanol (0.1%), chlorothalonil (0.2%) katika muda wa siku 15 kutoka hatua ya kuanza kwa maua inaweza kudhibiti ugonjwa huo. Unapotumia dawa, vaa nguo za kujikinga kila wakati na ufuate maagizo kwenye lebo ya bidhaa kama vile kipimo, muda wa matumizi, na muda wa kabla ya kuvuna. Daima, fuata kanuni za kikanda kuhusu udhibiti wa wadudu.

Ni nini kilisababisha?

Spishi za Elsinoë ni vimelea vya mimea vinavyo sababisha ukoko/upele kwenye mimea mingi, ikijumuisha baadhi ya mazao muhimu kiuchumi kama parachichi, michungwa, mizabibu, mimea ya mapambo, mazao ya shambani na miti shamba. Tafiti za ziada zinahitajika ili kuibua epidemiolojia ya ugonjwa huu na kubainisha athari halisi za kiuchumi katika uzalishaji wa kibiashara. Ukosefu wa maarifa ya epidemiolojia ni kwa sababu ya ukosefu wa miundo yenye rutuba ya vielelezo vya Elsinoë vilivyokusanywa kutoka kwenye mashamba yaliyoambukizwa. Inapaswa kuzingatiwa kuwa dalili zinazofanana na upele hupunguza soko la mazao, kwa hivyo utafiti zaidi unahitajika. Imeonekana kuwa hali ya hewa ya mvua husababisha kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.


Hatua za Kuzuia

  • Hatua za usafi wa mazingira zinapaswa kufuatwa kwa ulazima.
  • Majani yote yaliyoambukizwa, matunda yanapaswa kukusanywa na kuchomwa moto.
  • Kupogoa vijiti/matawi yenye ugonjwa ni muhimu ili kupunguza chanzo cha maambukizi.
  • Pamoja na utafiti zaidi juu ya epidemiolojia ya mdudu huyu maalum hatua bora zaidi za kuzuia katika komamanga zitapatikana.

Pakua Plantix