Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Doajani Phyllosticta la Mbaazi

Phoma cajanicola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda kwenye majani.
  • Madoa mengi madogo, meusi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Dalili

Vidonda vya mduara, vya mviringo na visivyo na umbo la kawaida au umbo la 'V' hutokea kwenye majani. Vidonda ni vya kijivu au hudhurungi na vina ukingo mwembamba, mweusi. Kwenye vidonda vya zamani, kuna vijidoa vingi, vidogo vyeusi (miili ya pycnidial, njia ya kusambaza vijimbegu vinavyozaliana bila muunganiko wa mbegu ya kiume na kike ).

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna mbinu za kibayolojia zinazojulikana kwa kudhibiti ugonjwa huu kwa mafanikio.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matumizi ya bidhaa zilizodhibitiwa yanapaswa kufanywa mara tu madoa yanapotokea kwenye majani.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na fangasi Phyllosticta cajanicola. Jenasi hii inapozaa kwenye majani inajulikana kama Phyllosticta wakati ikitokea kwenye sehemu nyingine za mmea hulikana kwa utaratibu kama Phoma. Kuvu huishi katika mabaki ya mazao yaliyoshambuliwa na inaweza kuambukizwa kupitia mbegu. Hali ya joto, unyevu huchochea maendeleo ya ugonjwa huu.


Hatua za Kuzuia

  • Fanya mzunguko wa mazao na kulima mara kwa mara ili kupunguza maisha ya Kuvu.

Pakua Plantix