Karanga

Doa la Pilipili na Kuungua

Leptosphaerulina arachidicola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Maeneo makubwa yaliyoungua yenye umbo la V hutokea kwenye ncha ya majani.
  • Doa la pilipili huonekana kama vidonda vidogo vyeusi (chini ya 1 mm) ambavyo hukua kwenye pande za juu za majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Karanga

Dalili

Awamu ya doa la pilipili ina sifa ya vijidoa vidogo vyenye tishu zilizo kufa kwenye majani ya chini karibu na usawa wa ardhi. Madoa ni mengi na yana ukubwa wa tundu la sindano. Kuungua hutokea wakati sehemu ya umbo la V ya jani inapokufa (kawaida kwenye ukingo) na ukanda wa njano huundwa karibu nayo.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Panda aina sugu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi pamoja na hatua za kuzuia na matibabu ya kibaolojia yanayopatikana. Weka dawa za kuua kuvu ambazo hutumika kudhibiti magonjwa mengine ya majani, kama vile chlorothalonil. Tumia dawa ya kuzuia kuvu ikiwa hakuna ugonjwa mwingine unaoathiri machaguo.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na kuvu aina ya Leptosphaerulina arachidicola, ambao huishi kwenye mabaki ya karanga na huenezwa na upepo. Pseudothecia huundwa kwa wingi katika tishu za jani zilizo kufa. Vipindi vya kilele vya mtawanyiko wa vijimbegu vilivyotolewa kwa nguvu hutokea mwishoni mwa kipindi cha baridi na mwanzoni mwa kipindi cha mvua.


Hatua za Kuzuia

  • Kuwa na mazoea ya kupanda mapema na kufanya mzunguko wa mazao.
  • Punguza kasi ya ongezeko la vimelea na kuenea.

Pakua Plantix