Fusarium/Pythium/Rhizoctonia complex
Kuvu
Dalili ya awali ya ugonjwa huonekana wakati sehemu ya juu ya mmea inapoanza kunyauka, ikifuatiwa na mchakato wa kugeuka njano na kufa kwa tishu, na kusababisha mmea kufa. Kudumaa kwa manjano au "ugonjwa wa rangi ya manjano" unaonekana kuchochewa na viwango vya unyevu kupita kiasi kwenye eneo la mizizi, na kusababisha ukosefu wa hewa kwenye mizizi. Katika muktadha huu, kuharibika kwa mizizi ya tumbaku kunapelekea kupenya au kubadilisha uwezekano wa mmea kupata uvamizi wa vimelea vinavyohusishwa na udumavu wa manjano.
Tumia aina za mimea ambazo ni sugu kwa vimelea vya magonjwa ya udongo.
Udumavu wa manjano hauwezi kudhibitiwa na kemikali na hutokea kutokana na usimamizi mbaya wa maji na udongo kujaa maji.
Tumbaku ina uvumilivu mdogo kwa upungufu wa O2 na CO2 iliyozidi. Na mchanganyiko wa unyevu kupita kiasi, ukosefu wa oksijeni na joto la juu unaweza kusababisha mfumo wa mizizi kuharibika. Kuharibika kwa mizizi ya tumbaku hupelekea kupenya kwa vimelea vya magonjwa kama vile Fusarium spp., Rhizoctonia solani, Pythium spp. nk ambvyo huhusishwa na udumavu wa manjano. Matokeo hutegemea mambo mbalimbali, kama vile hatua ya ukuaji, hali ya mazingira, muda na asilimia ya mizizi iliyoathirika.