Fusarium moniliforme
Kuvu
Ugonjwa hutokea katika hatua tatu kuu. Dalili za awali ni kuonekana kwa mabaka yaliyo badilika rangi kuelekea kwenye kitako cha majani machanga na mara chache kwenye sehemu nyingine za ubapa wa majani katika awamu ya kwanza. Majani hukunjana, kusokotwa na kufupishwa. Kitako cha majani yaliyo athiriwa mara nyingi ni kifupi kuliko majani ya kawaida. Awamu ya kuoza sehemu ya juu ni hatua mbaya zaidi ambapo uharibifu na kusokotwa kwa majani huonekana. Vibanzi vyekundu hupotea na kitako kizima cha msokoto huharibika na kukauka. Katika maambukizi makubwa, machipukizi ya pembeni huchipua na sehemu za ncha ya juu ya shina huharibiwa kabisa. Hatua ya tatu inayojulikana kama hatua ya mkato wa kisu inaonyesha mikato ya mshazari kwenye gome la bua au shina. Wakati majani yanapovuliwa, mabaka makubwa yaliyo badilika rangi yanaonekana kwenye mabua/shina.
Tumia aina sugu au sugu kiasi kwa upandaji ikiwa zinapatikana.
Daima zingatia mbinu jumuishi pamoja na hatua za kuzuia na matibabu ya kibaolojia yanayopatikana. Weka dawa za kuua kuvu, kama vile oksikloraidi ya shaba ili kupunguza ipasavyo ugonjwa wa pokkah boeng.
Uharibifu husababishwa na aina tofauti za Fusarium: Fusarium subglutinans, Fusarium sacchari, Fusarium moniliforme Sheldon. Viini hivyo vinaweza kuenezwa hasa na mikondo ya hewa na vijimbegu vinavyopeperuka hewani hutawala majani, maua na mashina ya mimea kupitia jeraha lolote la wadudu, vipekecha au nyufa za ukuaji wa asili. Maambukizi ya upili ni kupitia sehemu zilizoambukizwa, maji ya umwagiliaji, matone ya mvua na udongo. Maambukizi kawaida hutokea kupitia misokoto kando ya jani lililopanuliwa kwa sehemu. Vijimbegu vinavyoingia kwenye msokoto huota na kukua ndani ya tishu za ndani za jani la msokoto(majani yaliyo jiviriga kwenye ncha ya juu ya muwa inayokua). Hii husababisha kuharibika umbo na kufupisha majani. Kuenea kwa vijimbegu hutegemea hali mbalimbali za mazingira na hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi na kufuatiwa na msimu wa unyevu. Chini ya hali hizi, maambukizi ya majani hukua haraka, na hata aina sugu huonyesha dalili za kawaida za majani wakati mwingine. Vimelea vinaweza kuishi kwa muda wa miezi 12 katika uchafu wa mimea chini ya hali za asili.