Binzari ya manjano

Doa Jani la Bizari

Taphrina maculans

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa kadhaa madogo, ya mviringo, yasiyo na mpangilio yanaonekana kwenye nyuso zote za majani.
  • Madoa huungana na kuunda vidonda visivyo na mpangilio.
  • Mimea huonyesha mwonekano ulioungua na mavuno ya bizari hupungua.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Binzari ya manjano

Binzari ya manjano

Dalili

Ugonjwa huu kawaida huonekana kwenye pande za chini za majani. Madoa ni madogo yenye upana wa 1 - 2 mm na mara nyingi ni ya mstatili. Madoa yamepangwa kwa safu kando ya mishipa na huunganika kuunda vidonda visivyo na mpangilio. Kwanza, huonekana kama rangi ya manjano hafifu na baadaye kuwa manjano chafu. Majani yaliyoambukizwa yanaharibika umbo na kuwa na muonekana wa rangi nyekundu-kahawia. Katika hali mbaya, mimea huwa na muonekano wa kuunguzwa na mavuno ya bizari hupungua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Bidhaa zenye Pseudomonas fluorescens na Trichoderma harzianum zinaweza kupunguza maambukizi wakati shinikizo la ugonjwa liko chini. Kiziduo cha majani ya muashoki (Polyanthia longifolia) au kiziduo cha vitunguu pia kinaweza kupunguza uvamizi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Tibu mbegu kwa kutumia Mancozeb @ 3 g/lita ya maji au Carbendazim kwa 1 g/lita ya maji kwa dakika 30 na uzikaushe kabla ya kupanda.

Ni nini kilisababisha?

Kuvu huyu huenezwa hasa kwa njia ya upepo/hewa na maambukizi ya msingi hutokea kwenye majani ya chini. Viini vya kuvu hubakia kwenye majani makavu ya mmea ambayo huachwa shambani. Maambukizi ya upili husababishwa na vijimbegu ambayo huenea kutoka kwenye asci zilizo komaa na kuambukiza majani yenye afya. Katika majira ya kiangazi, vimelea hudumu kupitia seli za ascogenous kwenye uchafu wa majani na vijimbegu vilivyokauka na vijimbegu vya kwenye udongo na kati ya majani yaliyoanguka. Ugonjwa huu hupendelea unyevu mwingi wa udongo, joto la 25°C na unyevunyevu wa majani.


Hatua za Kuzuia

  • Zingatia usafi ipasavyo.
  • Kusanya na kuchoma majani yaliyoathirika na kavu ili kupunguza chanzo cha maambukizi shambani.
  • Chagua mbegu kutoka sehemu zisizo na magonjwa.
  • Fanya mzunguko wa mazao inapowezekana.

Pakua Plantix