Hyaloderma sp.
Kuvu
Ukuaji wa kuvu hutokea upande wa chini wa majani. Utokeaji wa madoa husababisha kupukutika kwa majani. Vidonda huenea kwenye majani yenye afya na kuungana na kuunda maeneo makubwa yasiyo na umbo maalum hadi maeneo ya umbo la nusu duara kwenye ubapa wa majani yenye kipenyo cha hadi milimita 4-5.
Hadi sasa, bado hakuna njia ya kudhibiti kibaiolojia inayojulikana.
Daima zingatia njia jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana. Kupulizia copper oxychloride (0 - 3%) wakati wa msimu wa mvua kunaweza kudhibiti ugonjwa.
Uharibifu husababishwa na kuvu/fangasi, ambae hushambulia majani yaliyokomaa katika hali ya kuloana. Katika hatua za juu zaidi na katika hali ya unyevu anga, ugonjwa unaweza kusababisha madoa makubwa kwenye majani karibu na lamima/ubapa wa jani.