Pestalotiopsis psidii
Kuvu
Ugonjwa huu kwa kawaida hujitokeza kwenye matunda mabichi na mara chache kwenye majani. Dalili za mwanzo za maambukizi kwenye matunda ni kuonekana kwa maeneo madogo, ya kahawia, yenye rangi mithili ya kutu na yaliyokufa tishu. Katika hatua za juu za maambukizi, maeneo yaliyokufa tishu huchana ganda la matunda na kuliacha wazi. Matunda yaliyoathirika ukuaji wake husimama, huwa magumu, yenye umbo lisilo la kawaida, na hudondoka.
Tumia mifuko yenye matundu mithili ya chandarua kufunika matunda ili kuzuia majeraha kwenye matunda.
Daima zingatia njia jumuishi zinazotumia hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana. Kupulizia mchanganyiko wa Bordeaux au copper oxychloride kunaweza kudhibiti kwa ufanisi kuenea kwa ugonjwa. Matumizi ya dawa za kuua wadudu kwenye matunda machanga baada ya uchavuaji kumeripotiwa kutoa matokeo mazuri.
Ugonjwa husababishwa na kuvu, na chanzo kikuu cha maambukizi ni kuvu bwete/tuli nyeupe iliyo mithili ya mtandao wa mizizi. Shambulio la haraka la kuvu husababisha uharibifu wa matunda. Maambukizi yanaweza kuenea kwa njia ya upili kupitia vijimbegu vya kuvu vinavyosafirishwa na upepo, matone ya maji, ukaribu na mimea iliyoambukizwa, majeraha, na usafirishaji wa majani yaliyoambukizwa. Kuvu inaweza kukua katika mazingira yenye unyevu anga kwa joto kati ya 20 na 25°C na sehemu yenye majani mengi na mtiririko wa hewa usio wa kutosha.