Tangawizi

Muozo wa Tangawizi

Pythium aphanidermatum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Majani ya manjano.
  • Mizizi iliyooza.
  • Tishu za tangawizi kubadilika rangi na kuwa za kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye

2 Mazao
Tangawizi
Binzari ya manjano

Tangawizi

Dalili

Maambukizi huanza kwenye eneo la kola ya shina bandia na kusambaa juu na chini. Eneo la kola ya shina bandia lililoathiriwa linakuwa na maji maji na kuoza kunasambaa hadi kwenye tunguu/tangawizi. Katika hatua ya baadaye, maambukizi ya mizizi pia huonekana. Dalili kwenye majani zinaonekana kama rangi ya manjano hafifu kwenye ncha za majani ya chini, ambayo huenea taratibu kwenye sehemu bapa za majani. Katika hatua za awali za maambukizi, sehemu ya katikati ya majani hubaki kuwa ya kijani huku kingo zikigeuka kuwa njano. Hali ya kuwa manjano hufuatiwa na majani kudondoka, kunyauka, na kukauka kwa shina bandia.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia samadi ya ng'ombe ambayo ni laini na yenye maji maji au mbolea ya maji baada ya kila uwekaji wa matandazo ili kuboresha shughuli za vijidudu na upatikanaji wa virutubisho. Tumia aina za mbegu zinazostahimili au kuvumilia magonjwa kwa ajili ya kupanda. Fanya mzunguko wa mazao kwa kupanda mahindi, pamba, au soya. Spishi za Trichoderma kama T. viride, T. harzianum, na T. hamatum zinajulikana kwa kuzuia ukuaji wa kuvu wanaosababisha magonjwa (gramu 40 kwa kila mita ya mraba).

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Tibu tangawizi za mbegu kwa kutumia mancozeb 0.3% kwa dakika 30 kabla ya kuhifadhi na kabla ya kupanda ili kupunguza matukio ya ugonjwa.

Ni nini kilisababisha?

Magonjwa husababishwa na kuvu wa Pythium aphanidermatum, ambao huzaliana kutokana na kuongezeka kwa unyevu wa udongo wakati wa mvua za pepo za kusi-magharibi. Kuvu huweza kuishi kwa njia mbili. Mosi, huishi kwenye matunguu/tangawizi zenye magonjwa zilizohifadhiwa kwa ajili ajili ya mbegu, na pili, kupitia vijimbegu/viiniyoga vilivyopumizika kama vile vijimbegu/viiniyoga vyenye kuta nene (chlamydospores) na vijimbegu/viiniyoga vilivyozalishwa kutokana na urutubishaji wa vijiyai vya kuvu (yaani, oospores) ambavyo hufika kwenye udongo kutoka kwenye tunguu (tangawizi) zilizoathirika. Machipukizi madogo ndiyo yaliyo hatarini zaidi kuathiriwa na vimelea na ugonjwa huo huongezeka zaidi kutokana na uvamizi wa minyoo. Joto la juu zaidi ya 30°C na unyevu mwingi wa udongo ni mambo muhimu yanayochangia kuenea kwa ugonjwa huo. Hali ya maji yaliyotuama kwenye shamba inayosababishwa na mfumo dhaifu wa kutoa maji shambani pia huongeza uzito wa ugonjwa.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha kunakuwa na mfumo mzuri wa kutoa maji, na chagua udongo usiotuamisha maji kwa ajili ya kupanda zao la tangawizi.
  • Tumia hatua za udhibiti wa magonjwa na wadudu waharibifu kama vile kuondoa na kuharibu mimea iliyoambukizwa.
  • Weka matandazo ya majani mabichi kiasi cha tani 4-4.8 kwa ekari wakati wa kupanda.
  • Rudia kiasi cha tani 2 kwa ekari kati ya siku 40 hadi 90 baada ya kupanda.
  • Fuata kilimo cha mzunguko wa mazao kwa angalau miaka 2-3.
  • Tumia keki ya mwarobaini kiasi cha gramu 250 kwa kila mita ya mraba na chokaa kama njia ya kurekebisha udongo.

Pakua Plantix