Hemileia vastatrix
Kuvu
Dalili ya awali ni kuonekana kwa doa la manjano lenye kipenyo cha milimita 2-3 kwenye majani ya mmea wa kahawa. Madoa hupanuka na kuwa madoa makubwa ya mviringo ambayo yanageuka na kuwa ya rangi ya machungwa angavu hadi nyekundu na hatimaye kuwa ya kahawia yenye kingo za manjano. Kwenye upande wa chini wa jani, madoa hayo huanza kutoa vijimbegu ambavyo huonekana kama unga wa rangi ya machungwa hadi kahawia. Hatimaye majani hudondoka kutoka kwenye mti. Kutokana na kukosekana kwa majani, usanisinuru hauwezi kufanyika, na mimea hukosa virutubisho na hivyo kuwa na mavuno kidogo ya kahawa.
Mbinu za kibiashara za udhibiti wa kibaolojia kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huu hazipatikani sana. Kuzingatia hatua za kinga kutatoa matokeo makubwa zaidi katika kudhibiti ugonjwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia yanayopatikana. Kinga ya kupulizia Bordeaux au Copper Oxychloride 50% WG inaweza kufanyika mara moja kabla ya kutokea mazingira muafaka ya ukuaji wa ugonjwa na mara nyingine baada ya kipindi hicho kumalizika.
Uharibifu husababishwa na kuvu Hemileia vastatrix. Kutu ya kahawa huenea haraka sana na sababu za kimazingira zina mchango mkubwa katika kuenea kwa kuvu. Njia muhimu zaidi ya kueneza kuvu ni kupitia upepo au maji. Husambazwa pale ambapo vumbi na vijimbegu vya kuvu vinapoenea katika shamba na kuambukiza shamba lingine, au vinapoanguka chini na kutapakaa kwenye mmea mwingine wakati mvua inaponyesha. Kutu ya kahawa hustawi katika mazingira yenye unyevunyevu na mvua inayodondokea kwenye majani huchangia kuenea kwa vijimbegu kutoka mti mmoja hadi mwingine. Matunda ya kahawa kutoka kwenye miti iliyoathirika yanaweza kuwa na ukuaji mbovu na kuwa nyepesi. Mlipuko wa kutu ya kahawa unaweza kusababisha upotevu wa mavuno kwa zaidi ya asilimia 75 pale ambapo milipuko ya ugonjwa ni mikubwa.