Phyllosticta zingiberis
Kuvu
Ugonjwa huanza kama madoa madogo, ya mviringo, yaliyotota maji kwenye majani machanga. Baadaye yanakuwa meupe katikati na ukingo mweusi uliozungukwa na mduara angavu wa manjano. Madoa yatakua, kuungana, na kuunda majeraha makubwa yanayotokana na kufa kwa tishu. Wakati sehemu kubwa ya jani inapofunikwa na majeraha, jani likauka na hatimaye hufa.
Hadi leo, hatufahamu uwepo wa njia yoyote ya udhibiti wa kibaiolojia dhidi ya ugonjwa huu. Ikiwa unafahamu njia yoyote iliyofanikiwa kupunguza matukio au ukubwa wa dalili za ugonjwa, tafadhali wasiliana nasi.
Daima zingatia njia jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Pulizia mchanganyiko wa Bordeaux au tumia dawa za kuua kuvu/ukungu zenye hexaconazole (0.1%), propiconazole (0.1%) au carbendazim + mancozeb wakati ugonjwa unapogunduliwa kwa mara ya kwanza, kisha rudia kupulizia majani mara mbili kila baada ya siku 20.
Dalili hizi husababishwa na kuvu wanaofahamika kama Phyllosticta zingiberis ambao husambazwa kwa udongo. Maambukizi ya awali hutokea kwa sababu ya uwepo wa vijimbegu vya kuvu kwenye udongo au kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa. Upepo na matone ya mvua husababisha maambukizi ya upili. Vimelea vya kuvu hustawi vizuri kwenye hali ya unyevu anga wa juu na nyuzijoto kati ya 20°C na 28°C. Ugonjwa unaweza kusababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi na ukubwa wa tangawizi. Majani yenye umri wa wiki mbili ndiyo yaliyo hatarini zaidi kuathiriwa.