Shayiri

Fugwe Funika ya Shayiri

Ustilago segetum var. hordei

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Punje nyeusi.
  • Vifuniko laini vya juu ya punje vilivyonyauka na kuharibika umbo.
  • Mimea iliyodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Shayiri

Shayiri

Dalili

Kwa kawaida mimea iliyoathirika haionyeshi dalili zozote hadi masikio yanapochomoza. Masikio yaliyoambukizwa huchomoza muda sawa au baadae kidogo kulinganisha na yale yenye afya. Mara nyingi masikio hujitokeza kupitia kifuniko/kifuko kilicho chini ya jani la mwisho (jani bendera). Dalili inayojulikana zaidi ni kubadilika kwa rangi ya punje, rangi ikigeuka kuwa nyeusi. Mbegu katika masikio yaliyoambukizwa hushikiliwa na utando mgumu wa kijivu-nyeupe. Karibu na mavuno, vijimbegu vya fungwe moja kwa moja huchukua nafasi ya mbegu za shayiri. Vifuniko laini vya juu ya punje huonekana kuharibika umbo. Mimea ya shayiri inaweza kudumaa katika ukuaji wake.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya mbegu kwa kutumia unga wa majani ya Vitex negundo yana ufanisi. Kutibu mbegu zako kwa tiba za vidhibiti vya kibaiolojia kama vile Trichoderma harzianum, T. viride, na Pseudomonas fluorescens, ufanisi wake ni hafifu katika kudhibiti ugonjwa huu ikilinganishwa na dawa za kuua kuvu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana. Udhibiti kamili wa ugonjwa ulipatikana kwa kutibu mbegu kwa kutumia carbendazim 50 WP (2.5 g), mancozeb 50 WP + carbendazim 50 WP (1 g), carboxin 37.5 WP + thiram 37.5 WP (1.5 g) na tebuconazole 2 DS (1.5 g) kwa kilo 1 ya mbegu.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizi husababishwa na vimelea vya Ustilago segetum var. hordei. Ni ugonjwa unaoenezwa nje ya mbegu, ikimaanisha kwamba vichwa vya mimea yenye ugonjwa hueneza vijimbegu vya ugonjwa kwenye mbegu zenye afya. Wakati makundi ya viinimbegu vinapopasuka na kuwa wazi wakati wa kupura shayiri baada ya mavuno, viinimbegu vingi hutoka. Viinimbegu vingi hushikamana na punje zenye afya na hubaki vimelala hadi mbegu zinapopandwa. Mbegu za shayiri zinapooanza kuota, viinimbegu navyo huota na kuambukiza miche. Udongo wenye joto, unyevunyevu, na asidi ni muafaka kwa maambukizi ya miche. Ugonjwa huu hupendelea joto la udongo la kati ya 10°C na 21°C wakati wa kipindi cha kuota. Fugwe funika wakati mwingine ni vigumu kutofautisha na fugwe funguka.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina ya mbegu ambazo ni sugu dhidi ya magonjwa ikiwa zinapatikana.
  • Tumia mbegu zisizo na magonjwa kwa ajili ya kupanda.
  • Panda mbegu zako kwenye udongo wenye ukavu wa wastani.
  • Matukio ya magonjwa yanaweza kupunguzwa kwa kupanda mbegu kwa kina cha sentimita 2.5.
  • Panda shayiri kwenye udongo huru (usio na asidi wala alkali), na ikiwezekana, iwe ni udongo wenye alkali badala ya udongo wa asidi.
  • Ondoa mimea iliyoathirika, ing’oa na ichome.

Pakua Plantix