Zabibu

Kutu ya Zabibu

Phakopsora euvitis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mkusanyiko wa vitu mithili ya unga wenye rangi ya kahawia-machungwa upande wa chini wa jani.
  • Udondokaji mapema (kabla ya wakati) wa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Zabibu

Dalili

Mwanzoni, mkusanyiko wa vitu mithili ya unga wenye rangi ya kahawia-machungwa unaweza kupatikana upande wa chini wa majani. Majeraha madogo yenye rangi ya manjano hadi kahawia baadae huonekana kwenye pande zote za jani. Kadri ugonjwa unavyoendelea kukua, mikusanyiko ya rangi ya machungwa hubadilika rangi na kuwa ya kahawia yenye weusi hadi inayokaribia kabisa kuwa nyeusi na kutengeneza majeraha yaliyorefuka. Uvamizi mkubwa wa vijidudu utaifanya miti yote kuwa ya rangi ya manjano au kahawia na hatimaye kusababisha kupukutika majani mapema. Katika msimu unaofuata wa ukuaji, mashina yatakuwa na ukuaji duni, na kusababisha kudumaa kwa ukuaji wa mizabibu. Ugonjwa unaweza kusababisha ukuaji duni wa shina, kupungua kwa ubora wa matunda, na upotevu wa mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Pulizia majani kwa dawa ya kuua kuvu yenye salfa. Epuka kupulizia wakati wa mvua ili kuhakikisha dawa ya kuua kuvu inaweza kupambana dhidi ya vimelea vya ugonjwa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia njia jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Tumia dawa za kuua kuvu zenye mchanganyiko wa Bordeaux, difolatan, propiconazole, tebuconazole au azoxystrobin, ambazo zinatajwa kuwa na uwezo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa vimelea vya ugonjwa. Kutu inaweza kudhibitiwa kwenye mashamba ya mizabibu kwa kupulizia Baycor (0.1%) mara 3-4 katika kipindi cha kila baada ya wiki mbili wakati wa msimu unaofuata wa ukuaji.

Ni nini kilisababisha?

Dalili za ugonjwa huu husababishwa na kuvu/fangasi aitwae Phakopsora euvitis. Vijimbegu vya kuvu huishi kwenye mabaki ya mimea na mimea mbadala inayohifadhi vijidudu, na husambazwa kwa njia ya upepo. Vimelea vya kutu vinakua kwenye madoa yaliyopo upande wa chini wa jani katika muundo wa vijichembe vyenye rangi ya machungwa. Mikusanyiko ya vijimbegu vyenye ukuta mwembamba (yaani uredinospores) vyenye rangi ya manjano ya machungwa vinazalishwa kwenye upande wa chini wa jani, vikiwa na madoa meusi yanayotokana na kufa kwa tishu kwenye upande wa juu. Joto lililo juu ya 20°C na hali ya hewa ya unyevu ndio mazingira muafaka kwa ukuaji wa ugonjwa. Vijimbegu vya kuvu vinaweza kusafirishwa kwa urahisi kwa upepo na mkondo wa hewa.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina ya mbegu zinazostahimili magonjwa, ikiwa zinapatikana.
  • Kagua mizabibu yako mara kwa mara ili kugundua uwepo wa dalili za kutu upande wa chini wa majani.
  • Kusanya na choma moto sehemu za mimea zilizoambukizwa.
  • Punguza (pogoa) mizabibu ili kuipatia mzunguko mzuri wa hewa.

Pakua Plantix