Epicoccum sorghinum
Kuvu
Dalili za mwanzo huonyesha madoa madogo, marefu, yenye umbo la mviringo ambayo yana rangi ya kijani kibichi hadi nyekundu-kahawia na halo ya manjano. Dalili za baadae zinajulikana kwa vidonda vikubwa na virefu vilivyo na mpangilio usio maalumu na kingo za rangi nyekundu-kahawia. Madoa yanaweza kuungana na kutengeneza mabaka makubwa, ambayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya rangi ya njano na kufa kwa tishu.
Tumia Calcium Silicate Slag kama marekebisho ya udongo ili kupunguza ukali wa doa la mviringo.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Mpaka leo, hakuna mbinu za udhibiti wa kikemikali ambazo zimetengenezwa dhidi ya fangasi hawa.
Uharibifu huo husababishwa na fangasi wa Epicoccum sorghinum, na huenezwa na viiniyoga vya kuvu vinavyo peperushwa na upepo au mvua. Kuvu anahitaji hali ya joto na unyevu ili kuongezeka. Kwa ujumla huathiri majani yaliyo komaa zaidi, kwa hiyo unachukuliwa kuwa ugonjwa mdogo wenye umuhimu mdogo wa kiuchumi.