Muwa

Mbabuko wa Jani la Muwa

Stagonospora sacchari

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Majani yanaonyesha madoa madogo yasiyo ya kawaida yenye rangi nyekundu-nyeusi yaliyo na mduara angavu wa manjano.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Muwa

Dalili

Dalili za awali ni ndogo zenye madoa meupe hadi manjano kwenye majani, na kwa kawaida hutokea kati ya siku 3 na 8 baada ya kuambukizwa. Madoa mekundu au mekundu-kahawia huonekana kwenye majani machanga na kurefuka polepole na kuwa umbo la pia na mduara wa manjano dhahiri. Katika hali ya ukali wa ugonjwa, madoa huungana na kuenea kando ya vitita vya mishipa hadi kwenye ncha ya jani na kutengeneza michirizi yenye umbo la pia/msokoto. Vidonda ni vyekundu-kahawia mwanzoni ambavyo baadaye hubadilika kuwa rangi ya majani makavu, iliyopakana na kingo nyekundu. Vishimo vya kuvu vidogo vyeusi pia hutengenezwa kwenye tishu zilizokuflea za jani. Majani yaliyoathirika sana hukauka na kuanguka mapema. Maambukizi hupunguza urefu wa bua/shina, kipenyo na idadi ya pingili, pamoja na idadi ya majani ya kijani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo, hatujafahamu mbinu yoyote ya kibaolojia inayopatikana dhidi ya ugonjwa huu. Ikiwa unajua njia yoyote iliyofanikiwa ya kupunguza matukio au uzito wa dalili, tafadhali wasiliana nasi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Weka dawa za kuua kuvu kama vile Carbendazim na Mancozeb. Nyunyizia mchanganyiko wa Bordeaux au Chlorthalonil, Thiophanate-methyl, na Zineb.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na vimelea vya kuvu wa Stagonospora sacchari, ambavyo husababisha kuungua sana na kupunguza sana shughuli za usanisinuru za mimea. Ugonjwa huu hutokea hasa baada ya mvua kunyesha au wakati umwagiliaji wa kupita unapo fanywa kwenye mashamba. Hii inasababisha kupunguzwa kwa eneo tendaji la jani. Ugonjwa huo hauwezi kuambukizwa kupitia udongo, vipandikizi vya miwa na zana za kilimo. Hasa huenezwa kupitia mtiririko wa hewa, upepo, na mvua. Katika hali ya hewa kavu, utokeaji wa michirizi ni wa haraka. Michirizi mingi huungana, kurefuka, kuzuia kukomaa na kubadilisha rangi ya tishu. Uundaji wa michirizi huonekana wazi zaidi wakati wa majira ya kuchipua na vuli, na wakati wa majira ya baridi kali, joto huwa chini sana kwa vimelea kuweza kuishi. Hatimaye, uso wote wa jani unaonyesha mwonekano wa kawaida ulio ungua/kubabuka.


Hatua za Kuzuia

  • Hatua za usafi husaidia kupunguza viwango vya maambukizi.
  • Panda aina sugu.
  • Ondoa wenyeji mbadala kama vile Saccharum spontaneum, Imperata cylindrica, na Rottboellia cochinchinensis.
  • Ondoa majani yaliyoambukizwa.
  • Upandaji unapaswa kufanywa wakati mvua na unyevu ni mdogo ili kupunguza matukio ya magonjwa.
  • Baada ya kuvuna, mashamba yaliyoathirika sana yanaweza kuchomwa moto ili kuua viiniyoga ndani ya vishimo vya kuvu kwenye uchafu wa mimea na kwenye udongo.
  • Weka mbolea za asili zaidi, fosforasi na potashi.

Pakua Plantix