Cercospora malayensis
Kuvu
Mwanzo, madoa ya kahawia yasiyo na mpangilio huonekana kwenye upande wa chini wa majani. Majani ya zamani, yaliyo karibu na ardhi huathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Majani hukauka na kuwa kahawia ugonjwa unapoendelea na huweza kujikunja na hatimaye kudondoka. Wakati wa mashambulizi makali, mmea unaweza kukauka kabisa. Mwanzoni, dalili za ugonjwa huonekana wazi kwenye uso wa chini wa majani kama madoa yasiyojulikana kwa namna ya madoa ya olivaceous. Baadaye, ukungu wa rangi ya kahawia nyepesi hadi kijivu hufunika uso mzima wa chini. Katika hali mbaya, madoa yenye seli zilizokufa yanaweza pia kuonekana kwenye uso wa juu wa majani. Majani yaliyoambukizwa hatimaye hukauka na kudondoka. Ugonjwa huendelea juu kutoka kwenye majani ya chini na huambukiza shina na matunda na huonesha dalili zinazofanana. Dalili zinaweza kufanana na zile za P. abelmoschi, ambae husababisha madoa meusi ya pembe.
Mpaka sasa, hatujafahamu mbinu yoyote ya kibaolojia inayopatikana dhidi ya ugonjwa huu. Ikiwa unajua njia yoyote iliyofanikiwa ya kupunguza matukio au uzito wa dalili, tafadhali wasiliana nasi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Nyunyizia dawa ya kuua kuvu kwenye upande wa chini wa majani mchana. Tumia dawa za kuua kuvu kama vile Copper oxychloride @ 0.3%, mancozeb @ 0.25% au zineb @ 0.2% mwezi mmoja baada ya kupanda na rudia utaratibu huu kila baada ya wiki mbili, kulingana na ukali.
Madoa ya majani husababishwa na fangasi Cercospora malayensis na Cercospora abelmoschi. Huishi msimu mzima kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa kwenye udongo na hivyo huambukiza mizizi na majani ya chini ya mimea ya bamia. Chavua/vijimbegu huenea mara ya pili kupitia upepo, mvua, umwagiliaji na zana za mitambo. Madoa ya majani hutokea sana wakati wa msimu wa unyevunyevu, kwani kuvu hupendelea hali ya hewa ya joto na mvua. Mvua na unyevunyevu mwingi hupelekea maambukizi, ukuaji wa magonjwa na kuenea kwa vimelea kwenye majani.